NJOMBE Siku chache baada ya shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii mkoa wa Njombe NSSF Kukabidhi msaada wa taa mbili kwaajili ya chumba cha upasuaji katika hospitali ya Kibena wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11,kwa mara nyingine tena Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi amepokea msaada wa mashuka na mablanketi sabi wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili. Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo mwenyekiti wa kwaya ya St.Joseph ya kanisa Katholiki Jimbo la Njombe bwana Mario Lugenge amesema kuwa msaada huo ni mwendelezo wa kanisa Katholiki kupitia kwaya mbalimbali za kanisa hilo kukabidhi misaada kwa watu wasiyojiweza,yatima na wagonjwa kama maandiko ya biblia yanavyosema. Aidha bwana Lugenge amesema kuwa kufanikisha zoezi hilo kumetokana na mapato ya mkanda a Vedeo ambao walitengeneza pamoja na kupata michango kutoka kwa wadau mbalimbali wa mkoa wa Njombe ambao waliichangia kwaya hiyo na kufanikisha kununua mashuka 35 na mablanketi 35 ambayo ni mazito kulingana na baridi ya msimu huu. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi mara baada ya kupokea msaada huyo ,Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Njombe bwana Hamisi Chindul ameshukuru kwa hatua hiyo na kuwaomba wanakwaya hao kuendelea na moyo wa kuwasaidia wasiyojiweza huku taasisi nyingine zikipaswa kuiga mfano huo kuwasaidia wagonjwa na vifaa vya hospitali hiyo. Bwana Chindul amewataka wauguzi wa hospitali hiyo kuvitunza vifaa mbalimbali ambavyo vimekuwa vikitolewa na watu wenye mapenzi mema kama msaada kwa wagonjwa na marekebisho ya hospitali ili mashirika na watu wenye moyo wa kusaidia hospitali hiyo wasikatishwe tamaa na utunzaji na matumizi ya vifaa hivyo. Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Kibena Dr James Ligwa akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe amepongeza kwa hatua hiyo ya kwaya ya St. Joseph kukabidhi msaada huo na kwamba atahakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo yaliokusudiwa na kuvitunza visiharibike. Hospitali ya mkoa wa Njombe ya Kibena imekuwa ikijipatia misaada mbalimbali kutoka kwa mashirika,taasisi na watu binafsi tangu ilipokabidhiwa kuwa ya mkoa ambapo siku chache zilizopita shirika la Hifadhi ya Jamii mkoa wa Njombe NSSF na makanisa mjini Njombe yameanza kupeleka misaada hiyo ili kuboresha mazingira yake na kuwasaidia wagonjwa baadhi ya huduma

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: