MABINGWA wa dunia, Hispania wameianza vibaya mno michuano ya Kombe la Dunia baada ya kutandikwa mabao 5-1 na Uholanzi usiku huu Uwanja wa Fonte Nova, Brazil. Hispania walikuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo wa Kundi B, mfungaji Xabi Alonso kwa penalti dakika ya 27 baada ya Stefan De Vrij kumchezea rafu Diego Costa ndani ya boksi Uholanzi ikasawazisha kupitia kwa Robin van Persie dakika ya 44 akimalizia pasi ya Daley Blind kumchambua kipa Iker Casillas. Uholanzi ikapata bao la pili dakika ya 53 kupitia kwa Arjen Robben aliyeumiliki vyema mpira kama Dennis Bergkamp alivyofanya dhidi ya Argentina katika Kombe la Dunia la mwaka 1998 Ufaransa, kabla ya kumtungua kwa shuti la kubabatiza Casillas. Kiungo Wesley Sneidjer akaifungia bao la tatu Uholanzi dakika ya 64 kwa shuti la mpira wa adhabu, kabla ya van Persie kufunga la nne dakika ya 73. Robben alihitimisha karamu ya mabao ya Uholanzi dakika ya 80 kwa bao zuri akikimbia kutokea katikati ya Uwanja kabla ya kuingia ndani na kumchambua Casillas akimuacha anagalagala chini na kutumbukiza mpira nyavuni. Kikosi cha Hispania kilikuwa; Casillas, Azpilicueta, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Alonso/Pedro dk63, Xavi, Busquets, Silva/Fabregas dk78, Diego Costa/Torres dk62 na Iniesta. Uholanzi: Cillessen, Janmaat, Vlaar, De Vrij/Veltman dk78, Martins Indi, Blind, De Guzman/Wijnaldum dk62, Sneijder, De Jong na Van Persie/Lens dk79.

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: