KIPA Gianluigi Buffon yuko kwenye hatihati kuidakia Italia katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia baada ya jana kuumia kifundo cha mguu mazoezini mjini Manaus. Buffon alitoka nje lakini kocha Cesare Prandelli bado ana matumaini Nahodha na mkongwe wake huyo atakuwa tayari kucheza dhidi ya England. Prandelli ana matatizo ya kutosha ya safu ya ulinzi akiwa tayari amempoteza beki wa kushoto chaguo lake la kwanza, Mattia di Sciglio wa AC Milan ambaye ni majeruhi. +8 Shakani: Kipa Gianluigi Buffon yuko hatarini kuukosa mchezo dhidi ya England Si maumivu makali ya kumfanya arejeshwe kabisa nyumbani, lakini yuko shakani kudaka katika mechi ya Kundi D mjini Manaus. Iwapo Buffon hatakuwa fiti kwa asilimia 100 litakuwa pogo kwa Italia, kwani mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 anayedakia Juventus, ndiye mchezaji aliyeichezea mechi nyingi zaidi Azzuri kihistoria, na amekuwa chaguo la kwanza karibu kwa miaka 15 sasa na alikuwemo kwenye kikosi kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2006 Ujerumani. Matokeo mabaya ya Italia katika fainali zilizopita Afrika Kusini inaaminika yalisababishwa na kukosekana kwake, baada ya kuumia katika mchezo wa kwanza.

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: