ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania


Hatimae
Wananchi wa Kijiji Cha Limage Wilayani Njombe Wameondokana na Tatizo la
Huduma ya Maji Safi na Salama Lililokuiwa Linawakabili Kwa Muda Mrefu
Baada ya Wananchi Hao Kuanza Kupata Huduma ya Maji ya Bomba.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Limage Emmanuel Mtedzi Amesema Kuwa Huduma ya Maji Kwa
Sasa Inapatikana Kwa Takribani Asilimia 80 Licha ya Mradi Huo
Kutokamilika Kwa Asilimia Mia Moja.
Amesema Kuwa Licha ya Mradi
Huo Kuanza Kutumika Lakini Bado Kunahitajika Zaidi ya Shilingi 271 Kwa
Ajili ya Kukamilisha Mradi Huo Ambapo Ulitakiwa Kukabidhiwa Kwa Wananchi
Mwezi Uliopita.
Aidha BwanaMtedzi Ameongeza Kuwa Kukamilika Kwa Mradi Huo Utawanufaisha Wakazi 1943 wa
Kijiji Hicho na Maeneo ya Jirani Waliokuwa Wakisafiri Umbali Mrefu Kwa Ajili ya Kupata Huduma ya Maji Safi na Salama.
Akielezea
Baadhi ya Changamoto Zinazojitokeza Mwenyekiti Huyo Amesema ni Pamoja
na Uharibifu Unaofanywa na Baadhi ya Wananchi na Watoto Ambao Wanakata
Mabomba Huku Akiwataka Wananchi Kuitunza Miundombinu ya Maji.
Upatikanaji
wa Huduma ya Maji Imetokana na Jitihada za Michango ya Wananchi Kwa
Kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Njombe Ambapo Machi 18 Mwaka Huu
Wakati wa Wiki ya Maji Diwani wa Kata ya Yakobi Bi.Ester Mgeni Aliweka
Jiwe la Msingi Katika Mradi Huo wa Maji .
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment