ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Serikali ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyomtoa mtafsiri wa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbu kumbu kifo cha Nelson Mandela imekuwa akidanganya kwa miaka mingi na imekuwa itoa watafsiri wenye kiwango cha chini.

![]() |
Thamsanqa Dyantyi mtafsiri wa lugha za ishara anayelalamikiwa |
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo siku ya jumanne.
Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane - Zulu amesema
hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri
huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali.
Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa.
Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo ametupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu.
Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya
viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana
Dyantyi kutoka kampuni ya SA Interpreters.
"Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kulikuwa kigumu sana kwake," alisema Waziri huyo.
0 comments:
Post a Comment