ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
MWANAMKE anayefahamika kwa jina la mama Eric, hivi karibuni muda wa saa
11jioni alijikuta akijifungua mtoto wa kiume Barabara ya Posta jijini
hapa kufuatia kushikwa na uchungu ghafla.
Akina mama waliomsaidia mama Eric kujifungua wakiwa na mtoto aliyezaliwa. |
Akiwa katika hali ya kuhangaika kusukuma mtoto, mwanamke huyo
aliishiwa nguvu huku tayari kichwa cha mtoto kikiwa kimetokeza nje,
ndipo mama mmoja aliyekuwa akisafiri akajitokeza kumsaidia kumzalisha.
“Nilimwona akihangaika kusukuma mtoto, lakini akaishiwa nguvu. Nilimwonea huruma nikatua begi na mkoba, nikamshika mikono akaja mama mwingine tukasaidiana kumzalisha,” alisema mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Euphrazia John, mkazi wa Bariadi, Simiyu.

Euphrazia alisaidiana na akina mama wengine, Juliana Wambura na mke wa diwani wa zamani wa Kata ya Nyamagana, Mama Mkiwa.
Mama Eric akiwa kwenye gari kuelekea nyumbani. |
0 comments:
Post a Comment