Tukio
hilo lilizua hofu kwa wakazi wa Mji wa Geita huku waliowengi wakitaka
kujua mtoto huyo aliyekutwa amefariki dunia baada ya kupotea kwa siku
nne mwaka 2011 na mwili wake kuzikwa, inakuwaje leo hii anaonekana akiwa
hai?
Tukio
hilo lililotokea Septemba mwaka huu linashuhudiwa na wazazi wa Shaban,
ndugu zake, jamaa na hata majirani wa eneo hilo ambao pia wanahoji, je
aliyezikwa wakati mwili wa mtoto huyo ulipookotwa ni nani na je mwili
wake uko kaburini au la?
Maswali
haya na mengine, yalikosa majibu kwani baada ya kuonekana kwake, Shaban
hakuweza kuongea vizuri na alionekana kutofahamu kabisa Kiswahili,
lugha ambayo kabla ya kutoweka kwake aliifahamu vyema. Wakati huu mtoto
huyu anaongea Kiha, japo nayo kwa tabu.
Hali
hiyo iliwalazimisha wazazi wake kushirikiana na Jeshi la Polisi
kumpeleka Haospitali ya Wilaya ya Geita ili apatiwe matibabu, lakini ni
kama hawakuona mtoto wao akipata nafuu hivyo waliondoka naye na kuamua
kumpeleka Kigoma Kambako anapatiwa tiba za jadi.
“Niliamua
nimpeleke kwa waganga wa jadi huku nyumbani Kigoma na sasa hali
inaendelea vizuri kwani anaweza kuongea japo ni kwa muda mfupi kisha
hunyamaza”, alisema baba mzazi wa mtoto huyo, Maulidi.
Shaban alikuwa wapi?
Shaban
hivi sasa anaendelea vizuri na ‘tiba’ anayopata huko Kigoma na aliweza
kuzungumza na gazeti hili kwa simu, huku akieleza kutoweka kwake, pia
huko alikokuwa kwa miaka mitatu, huku akiweka bayana kwamba hivi sasa
anawatambua vizuri
wazazi na ndugu zake.
Alisema
anakumbuka Januari 1, 2011 aliondoka nyumbani kwao na kuelekea
malishoni kuchunga mbuzi, na wakati akiwa machungani ghafla lilitokea
kundi la watu ambalo lilimzunguka.
Shabani
anasema katika kundi hilo alikuwamo mwanamke ambaye hakumtaja kwa
maelezo kwamba anashindwa kutamka jina lake, ambaye alimshika mkono na
kumtaka waondoke eneo hilo.
“Walikuja
watu wengi wanaume kwa wanawake, ghaflla walinizunguka na nikasikia
kama kizunguzungu na akili yangu ikawa kama imezubaa,”alisema Shaban na
kuongeza kuwa baada ya watu hao kumzingira walimwamuru aswage mbuzi zake
na kuwarudisha nyumbani.
Alitowekaje?
“Niliongozana
na watu hao tukiswaga mbuzi hadi nyumbani, lakini wakati nafika hapo
nyumbani hawakuweza kuniona japo mimi nilikuwa naona kila jambo lilikuwa
likiendelea,”anasimulia Shaban na kuongeza:
“Hao
watu walionizingira walijibadili sura na kuonekana kama majirani zetu
na mimi pia nilikuwa katikati ya kundi holo ila wazazi hawakuweza
kunitambua.
Alisema
kuwa baada ya kukabidhi mbuzi hao, watu hao waliondoka na yeye alibaki
pale nyumbani akiwa na mwanamke aliyemshika mkono, lakini wakati huo
hakuwa akionekana wazi wala kutambuliwa.
“Tulikaa
pale nyumbani kwa nusu saa tangu tulipofikisha mbuzi na baadaye
tuliondoka na huyo mwananke ambaye alikuwa amenishika mkono, na tukarudi
nilikokuwa nachungia na hapo tuliwakuta wale watu wengine wakiwa
wamesimama karibu na dimbwi la maji,”alisema Shaban.
Alisema
baada ya kufika katika dimbwi hilo walisimama katikati ya maji na
baadaye alishtukia akiwa chini ya bahari, ambako kulikuwa na senta
(kituo) kubwa na watu wengi wakiwa wanafanya shughuli mbalimbali.
“Tulisimama
katikati ya dimbwi la maji, gafla nilistukia niko katikati ya senta
kubwa ambayo iko ndani ya maji kama ziwa,”alisimulia mtoto huyo na
kuogeza kuwa eneo hilo kubwa kama mji ama kijiji ambako watu wanaishi.
Hata hivyo kila alipotaka kutaja watu hao alishindwa kutamka.
“Kunawatu
wengi kwenye eneo hilo na mimi nilistukia tu nikiwa huko na watu
wenyewe sikuwajua kwani walikuwa wageni kwangu,”alisema Shaban.
Hata
hivyo alipohojiwa wakati akiwa huko alikuwa akifanya nini, akila nini
na watu wanaoishi huko wanafanya shughuli gani, alishindwa kuongea na
kumkabidhi baba yake simu.
Kwa
upande wa baba yake huyo anasema tangu alipompeleka mwanaye Shaban kwa
mganga wa jadi aliyemtaja kwa jina la Seleman Bundala, aliyeko Kijiji
cha Nyankintonto, Kigoma amekuwa akipata nafuu.
Alisema
toka waanze matibabu ya jadi kumekuwa na mabadiliko makubwa kwani,mtoto
huyo alikuwa haongei, lakini kwa sasa anaongea japo kwa shida na kwamba
anaeleza alikokuwa na jinsi alivyopelekwa.
“Hatoi
maelezo mazuri kwani kunawakati anaongea vizuri na wakati anaonekana
kama ulimi unakuwa mzito hasa tunapomuuliza maswali kwamba ilikuwaje
akatoka huko na alikuwa akifanya nini na watu waliomchukuwa ni akina
nani,”alisema Maulidi.
Alitowekaje?
Maulidi
alitoweka ghafla Januari 1, 2011. Wazazi wake wanasema siku hiyo
aliondoka nyumbani asubuhi na kupeleka mbuzi malishoni, na kwamba siku
hiyo hakurudi, jambo lililowatia mashaka wazazi wake hivyo kuamua kutoa
taarifa polisi na kwa uongozi wa kijiji.
Taarifa
za kupotea mtoto huyo zilienea kijijini hapo na ndipo walianza juhudi
za kumtafuta na baada ya siku nne, alikutwa amekufa ndani ya kisima cha
maji.
“Mtoto
wetu aliondoka kwenda kulisha mbuzi siku ya sikukuu ya mwaka mpya muda
wa saa nne asubuhi, hadi inafika saa 12 jioni hakuonekana na badala yake
tuliona mbuzi wakiletwa na watoto wa majirani,”alisema Aziza Ramadhani
mama mzazi wa Maulidi.
Aziza
ndiye alikuwa wa kwanza kumtambua mtoto wake katika Mtaa wa Mbugani
eneo la Majarubani na wakati huo alikuwa akitoka kwenye shughuli zake za
kibiashara. Anasema alimwona Shaban akikatiza barabara.
“Nilimuona
mwanangu akiwa anakatiza njiani ndipo nilimuita, Shabani mwanangu ni
wewe? Niliposema hivyo alishtuka, nikaamua kumsogelea huku nikimwita
jina lake ndipo alipoitika lakini hakunitizama usoni,” alisema mama huyo
na kuongeza:
“Baada
ya kuthibitisha kwamba ndiye, watu walijaa na ndipo kwa kushirikiana na
majirani tulitoa taarifa polisi, na polisi wakaja kumchukua na
kumpeleka hospitali huku akiwa haongei na tulitumia ishara kuwasiliana
naye”.
0 comments:
Post a Comment