- Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku, imemsimamisha kazi Mwenyekiti, Ismail Aden Rage kutokana na masuala kadhaa, lakini kubwa imeelezwa ni suala la mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi.
- Kocha Mkuu Abdallah Kibaden na msaidizi wake Jamhuri Kikwelo "Julio" wameondolewa kazini baada ya kamati ya utendaji iliyokutana jana kufikia uamuzi kwamba wawili hao utendaji wao si sahihi.
- Simba sasa imemchukua kocha Zdravko Logarusic raia wa Croatia. Tayari Simba imemaliza mazungumza na kocha huyo na anatarajia kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kusaini mkataba na mara moja kuanza kazi. Kabla ya hapo, Logarusic alikuwa kocha wa Gor Mahia ya Kenya aliyoifundisha kwa misimu miwili akisha nafasi ya pili. Msimu huu ulikuwa wa mwisho, lakini aliondoka katikati na nafasi yake kuchukuliwa na Bobby Williamson ambaye kuna gazeti liliandika anajiunga na Simba, kitu ambacho hakikuwa sahihi. Baadaye Bobby alikanusha kuwa amefanya mazungumzo na Simba na ataendelea kubaki Kenya.
- Aliyekuwa akikaimu nafasi ya Umakamu Uenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are ‘Mzee Kinesi sasa ndiye mwenyekiti mpya Simba. Itang’are alikuwa akikaiumu nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Kaburu aliyeamua kuachia ngazi. Sasa ndiye atakuwa mwenyekiti mpya wa Simba, saa chache tu baada ya mwenyekiti, Ismail Aden Rage kusimamishwa. Mmoja ya wajumbe wa kamati ya utendaji, Swed Nkwabi yeye ameteuliwa kuwa kaimu makamu mwenyekiti.
- Selemani Matola ndiye kocha msaidizi mpya wa Simba anayechukua nafasi ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’. Uongozi wa Simba umethibitisha hilo leo kwamba Matola ndiye atasaidiana na Kocha Mkuu mpya, Zdravko Logarusic kutota Croatia. Uongozi wa Simba umethibitisha hilo ikiwa ni dakika chache baada ya kuwatimua kibaruani Kibadeni na Julio. Matola amekuwa akifanya kazi ya kukinoa kikosi cha Simba B ambacho kinashiriki michuano ya Uhai.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment