BAO
pekee la Mange Chagula dakika ya nane, limetosha kuipa ushindi wa
kwanza Azam FC katika michuano ya timu za vijana za klabu za Ligi Kuu,
chini ya umri wa miaka 20 maarufu kama Kombe Uhai, dhidi ya
JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Ushindi huo unafufua matumaini ya Azam kutetea taji hilo, baada ya kuanza awali kuanza vibaya kwa kufungwa mabao 2-1 na Azam, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Ulikuwa mchezo mkali wenye ushindani na burudani nzuri ya soka ya kufundishwa, uliohudhuriwa na watazamaji wachache.
Katika mchezo mwingine asubuhi ya leo, Yanga SC imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza Coastal Union ya Tanga bao 1-0, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Shujaa wa Yanga SC leo alikuwa ni Hamisi Issa aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 67 akimalizia pasi ya Hassan Kidishi.
Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Watoto hao wa Jangwani, baada ya awali kuilaza Mbeya City bao 1-0 kwenye Uwanja huo huo.
Kocha wa Yanga B, Salvatory Edward Augustino ‘Doctor’ alifurahishwa na matokeo hayo na kusema kwamba vijana wake wamecheza mechi ngumu mno mwanzoni, lakini wamefanikiwa kushinda.
“Kama ambavyo umeona mechi zetu zote tulizocheza ni ngumu, Mbeya City ni timu nzuri sana na leo Coastal umewaona ni wazuri, lakini wote tumewafunga, nina kila sababu ya kuwapongeza vijana wangu,”alisema kiungo huyo wa zamani wa Yanga.

0 comments:
Post a Comment