Mkuu wa Wilaya
ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi amewataka wananchi wa wilaya hiyo hasa vijijini
kuchangamkia fursa ya kuweka umeme nuru utokanao na jua
maalufu kama sola, ilikuboresha maisha yao na maendeleo kwa ujumla.
|
Mhandisi magessa akizungumza kuhusu mfumo wa jua |
Kipozi alisema
hayo mjini hapa juzi wakati wa hafla ya kufungua mafunzo maalumu ya umeme huo
kwa mafundi umeme, wadau na wauzaji wa vifaa vya umeme na vijana mbalimbali
ndani ya wilaya hiyo ambapo mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA).
Akielezea
kufarijika na mafunzo hayo ndani ya Wilaya yake, Kipozi alisema “Ni fursa ya
kipekee kwa wanamafunzo kutumia ujuzi huu kwani utaboresha maisha
yenu na pia kwa vijiji vitanufaika na umeme huu wa nuru” alisema.
Na kuongeza kuwa, kwa
fursa hiyo, anaamini matumizi ya kukata miti hovyo itapungua na baadala
yake wananchi watanufaika na huduma hiyo endapo wataichangamkia.
“Nawaomba wananchi
hasa mulio vijijini kuchangamkia fursa hii ya umeme nuru, pia nawapongezeni
wakufunzi na wandaaji kwa kuja muda muafaka kwani mafunzo
haya ni mipango endelevu ambayo itasaidia kusambaza teknolojia ya nishati
mbadala vijijini sambamba na kuwahamasisha wananchi kutumia nishati zitokanazo
na teknolojia ya nishati jadilifu” alimalizia Kipozi.
Kwa upande wake, mkuu
wa mafunzo hayo ya umeme nuru, Mhandisi, Finiasi Magessa alisema mafunzo
hayo yatasaidia kuboresha maisha ya watanzania mbalimbali hasa wa
vijijini ilikufikia malengo ya MKUKUTA, ili kila Mwananchi apate umeme wa
uhakika na gharma nafuu ifikapo 2015.
Aidha, wanamafunzo
wanatarajia kufaanya kwa vitendo kwa kufunga umeme nuru katika
shule na nyumba za walimu za Sekondari Kiwangwa, Matipwili na
Kibindu, huku mafunzo hayo yakitaraajia kumalizika Novemba Sab, mwaka huu.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment