WASANII WAMLIZA TENA MAMA KANUMBA



WASANII wa Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi waliofika kuzuru kaburi la aliyekuwa legendary wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, wameibua simanzi upya na kumsababisha mama wa marehemu, Flora Mtegoa kuangua kilio upya kwa mara nyingine.

Tukio hilo lililogusa hisia za watu wengi lilitokea Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar
SOMA ZAIDI...............

ambapo wasanii hao walifika kutoa heshima zao baada ya kushindwa kufika tangu nguli huyo alipofariki dunia Aprili 7, mwaka jana.

Wakiwa makaburini hapo wakiongozwa na baadhi ya waigizaji wa Kibongo, wasanii hao walionesha hisia kali huku wakishindwa kujizuia ambapo waliangua vilio, kitendo ambacho kilimfanya mama Kanumba naye aanze kulia kabla hajamuombea sala marehemu…

WASANII wa Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi waliofika kuzuru kaburi la aliyekuwa legendary wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, wameibua simanzi upya na kumsababisha mama wa marehemu, Flora Mtegoa kuangua kilio upya kwa mara nyingine.
Tukio hilo lililogusa hisia za watu wengi lilitokea Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo wasanii hao walifika kutoa heshima zao baada ya kushindwa kufika tangu nguli huyo alipofariki dunia Aprili 7, mwaka jana.
Wakiwa makaburini hapo wakiongozwa na baadhi ya waigizaji wa Kibongo, wasanii hao walionesha hisia kali huku wakishindwa kujizuia ambapo waliangua vilio, kitendo ambacho kilimfanya mama Kanumba naye aanze kulia kabla hajamuombea sala marehemu mwanaye.
“Mwanangu pumzika kwa amani huko uliko, mama yako bado nina maumivu,” alisikika mama Kanumba huku akiangua kilio kwa uchungu.
Wakati mama Kanumba akiendelea kulia, baadhi ya wasanii wa Bongo, Haji Adam ‘Baba Haji’, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ na Hashim Kambi ‘Wingo’ walilazimika kumbembeleza mama huyo huku nao wakilia.
Mbali na kuzuru kaburi la marehemu Kanumba wasanii hao kutoka nje ya Bongo, Sinia (Rwanda), Joy Liz (Kenya), Okuyu (Uganda) na wengineo, walitinga nchini kurekodi filamu ya Wekeza Inalipa kisha kurejea nchini kwao.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: