TAZAMA AYA MAAJABU MWANZA :WAJAWAZITO WANYWESHWA MAJI YA MBWA ALIYEJIFUNGUA PAMOJA JASHO LA WAUME ZAO

 
   Imani za kimila wilayani Misungwi mkoani Mwanza zinadaiwa kusababisha baadhi ya wajawazito kunyweshwa maji machafu yakiwemo yaliyofuliwa shati la mume husika anayetuhumiwa kufanya ngono wakati mke akiwa mjamzito, kwa kile kinachodaiwa ni kuondoa mkosi ili mjamzito husika ajifungue salama.

Katika jamii ya wenyeji wilayani hapa, ni kwamba mjamzito anaposhiriki katika tendo la ndoa na wanaume wengi, hupata kifafa cha mimba siku ya kujifungua na dawa yake ni kunyweshwa maji yaliyolowekwa mchanga kutoka eneo alilowahi kuzalia mbwa.
soma zaidi.................

Hayo yalielezwa katika mafunzo ya afya yanayoendelea wilayani hapa. Kuhusu kunyweshwa maji yaliyofulia shati, Mhudumu wa Afya katika Kijiji cha Mwamanga, Manyanda Kanyumbo alisema ikitokea mjamzito akachelewa kujifungua na ikagundulika mumewe alikuwa na uhusiano na wake wengi, shati lake hufuliwa na kisha mjamzito huyo hunyweshwa maji yaliyotumika.

“Watu wanaamini akishakunywa maji machafu ya mumewe hujifungua haraka na salama na kikombe alichonywea hufunikwa uvunguni mwa kitanda hadi atakapojifungua”, alisema.

Kwa upande wa mjamzito aliyetembea na wanaume wengi, jamii inaamini kwamba ili aweze kujifungua salama, lazima uchukuliwe mchanga sehemu ambayo mbwa amewahi kuzalia, ulowekwe kwenye maji na kisha mjamzito husika anywe kuondoa mkosi kabla ya siku ya Katika mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na hospitali ya Aga Khan kwa kushirikiana na Chuo cha Maendeleo na Ushirika cha MS TCDC kilichoko jijini Arusha, Kanyumbo alisema, “wanaamini kabisa mwanamke ambaye amechangia wanaume wengi, siku ya kujifungua kuna uwezekano mkubwa wa kupata kifafa cha mimba”.

Kanyumbo aliendelea kusema, “ili aweze kujifungua salama, bibi hufuata mchanga wa sehemu aliyozalia mbwa na kuuloweka kisha humnywesha, maana tunaamini mbwa hukutana na mbwa wengi ili aweze kutunga mimba, wale mbwa wengi huwafananisha na wanaume wengi.”

Jacqueline Martin muuguzi wa Mwanangwa, alisema baadhi ya watu wanaamini mjamzito akivuka mto, mtoto wake hazaliwi mapema na pia mwanamke huyo haruhusiwi kunywa maji akiwa amesimama.

Wanadai akinywa maji akiwa amesimama siku ya kujifungua, mtoto hawezi kushuka haraka.

Vile vile wanaamini mjamzito akikaa kwenye jiwe au kinu, mtoto huchelewa kuzaliwa. --- via HariLeo
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: