Zambia yaridhia pombe zake kali kupigwa marufuku Mbeya
- Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais wa Jimbo la Muchinga
nchini Zambia, Charles Sipanje akiwa jijini Mbeya juzi, alisema pombe
hizo, zilishapigwa marufuku kutengenezwa nchini mwao.
- Sipanje alisema, viroba hivyo maarufu kwa jina la ‘Tujilinjili’ nchini Zambia, vinauzwa Tanzania baada ya watengenezaji wake kupata soko la nje.
- Sipanje alisema, viroba hivyo maarufu kwa jina la ‘Tujilinjili’ nchini Zambia, vinauzwa Tanzania baada ya watengenezaji wake kupata soko la nje.
Mbeya. Serikali ya Zambia
imeunga mkono tangazo la kupiga marufuku uuzwaji wa pombe kali
zilizofungwa kwenye vikaratasi vya nailoni maarufu kama viroba.
Hivi
karibu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro , kwa niaba ya Kamati ya
Ulinzi na Usalama, alipiga marufuku uuzwaji wa pombe kutoka Zambia na
Malawi akisema zinaharibu nguvu kazi na kusababisha kero nyingi kwa
vijana.
Pombe hizo za viroba zilizopigwa marufuku ni pamoja na; Double Punch, Power No 1, Boss, Royal Punch na Charger.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais wa Jimbo la Muchinga nchini Zambia, Charles
Sipanje akiwa jijini Mbeya juzi, alisema pombe hizo, zilishapigwa
marufuku kutengenezwa nchini mwao.
Sipanje alisema, viroba hivyo
maarufu kwa jina la ‘Tujilinjili’ nchini Zambia, vinauzwa Tanzania baada
ya watengenezaji wake kupata soko la nje.
“Sisi tunaruhusu pombe
za aina hiyo ziwe kwenye chupa kubwa na siyo karatasi. Hivyo ni halali
kwa viongozi wa Mbeya kupiga marufuku,’’ alisema.
Pombe kali
zilizofungwa kwenye karatasi hizo zinadaiwa kuuzwa kwa kati ya Sh100 na
Sh 700, jambo linalosababisha watu wengi, wakiwamo watoto na madereva
kunywa bila kuzingtia taratibu na sheria za nchi.
Tayari vifo
kadhaa vinavyodaiwa kusababishwa na pombe za aina hiyo vimeripotiwa,
kikiwamo cha hivi karibuni ambapo mtu mmoja alifariki baada ya kunywa
pombe nyingi kwenye mkesha wa Mbio za Mwenge, wilayani Rungwe.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment