Wakati zoezi la kuhesabu kura linaendelea, taarifa zinaeleza Jamal Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF.
Hali hiyo inatokana na kawaida ya uchaguzi inavyokuwa kwamba
wajumbe waliokuwa katika kambi ya Malinzi kama Wilfred Kidau, Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ na wengine wameshinda.
Katika uchaguzi wa TFF imekuwa ni kawaida kwa hali hiyo kutokea
kwamba wajumbe wengi wa kambi moja wakishinda, basi ndiyo aliyekuwa
upande wao akigombea urais anaibuka na ushindi.
Taarifa kutoka ndani ya chumba cha upigaji kura zinaeleza wengi wao
wamempigia kura Malinzi hali iliyofanya Nyamlani asome alama za nyakati
na kuamua kuondoka ukumbini.
Habari kamili tutawaletea kadri zitakavyopatikana, stay tuned…………..
Mgombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi unaoendelea kwenye ukumbi wa NSSF Water Front mida hii, Athumani Nyamlani akiondoka zake kabla ya matokeo kutangazwa. Nyamlani alisema anakwenda kula, lakini habari kutoka ndani ya ukumbi wa Mkutano zinasema mpinzani wake Jamal Malinzi ameshinda kwa kishindo. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa baadaye usiku huu. |
Nyamlani akisindikizwa na wapambe wake kuondoka ukumbini |
Akisalimiana na wadau |
Alikuwa akisema asante akiambiwa pole na hongera |
0 comments:
Post a Comment