Kiungo
wa Arsenal na timu ya taifa ya England Jack Wilshere amepinga wazo la
kutoa uraia kwa wachezaji wasio na asili ya England na kutoa fursa ya
kuichezea timu ya taifa ya England .
Wilshere
alizungumza hayo wakati anajibu maswali ya waandishi wa habari juu ya
mawazo ya kocha wa England Roy Hodgson ambaye amevutiwa na kipaji cha
kiungo wa Manchester United Adnan Januzaj hadi ya kufikiria kumshawishi
aichezee England .soma zaidi,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Wilshere
amesema kuwa England inapaswa kuwakilishwa na wachezaji waliozaliwa
England pekee na si wahamiaji kwa kuwa hawawezi kuwa na asili ya utaifa
kama waliyo nayo wachezaji waliozaliwa England .
Mawazo
ya Wilshere yamepingwa na kocha wa timu ya taifa ya vijana ya England
Gareth Southgate ambaye kikosi chake kina wachezaji watano ambao sio
wazaliwa wa England .
Jamii
ya wanamichezo ya England ikiongozwa na nahodha wa zamani wa timu ya
taifa ya Cricket ya Ungereza Kevin Pietersen imempinga vikali kiungo
huyo wa Arsenal kwa kile kinachoonekana kama ubaguzi .
Pitersen
ambaye sio mzaliwa wa England alizaliwa nchini Afrika Kusini lakini
aliiwakilisha England na kuipa mafanikio makubwa kwenye mchezo wa
kriketi.
Zaidi
ya Pitersen yupo mwendesha baiskeli Chris Vroome ambaye alizaliwa
nchini Kenya na kukulia nchini Afrika ya kusini lakini anaiwakilisha
England kwenye mashindano ya baiskeli na mapema mwaka huu alishinda
ubingwa wa mashindano ya Tour De France.
Pitersen
alipinga mawazo ya Wilshere kupitia mtandao wake wa twitter ambapo
alimhoji kiungo huyo kuwa mawazo yake juu ya wanaopaswa kuiwakilisha
England yanamhusu yeye (Pietersen) ambaye ni mfano mzuri wa Muingereza
ambaye hakuzaliwa nchini Humo.
Wenzie
Wilshere wanaocheza naye kwenye timu ya taifa wametoka kwenye sehemu
tifauti tofauti lakini hii leo wana uraia wa England.
Wachezaji
kama Wilfred Zaha , Raheem Sterling , Saido Berahino na Nathaniel
Chalobah wamezaliwa nje ya England ambapo Zaha amezaliwa Ivory Coast ,
Chalobah amezaliwa Sierra Leone , Sterling amezaliwa Jamaica , Berahino
amezaliwa Burundi lakini wote wanaichezea England hii leo.
Wanamichezo wengine
maarufu kama Mo Farah ambaye ameiwakilisha England kwenye riadha ambapo
ametwaa medali kadhaa za dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki na
mashindano ya dunia pamoja na ya ulaya lakini si mzaliwa wa England .
0 comments:
Post a Comment