CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendeleza wimbi
lake la kubomoa ngome za Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kigogo wa
chama hicho na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Mbeya, Juma
Mwalunga, kujivua gamba la CCM na kuvaa gwanda la CHADEMA.
Kigogo huyo mwenye kadi namba 225, mjumbe wa Halmashauri Kuu mkoani hapa, amejiunga CHADEMA kwa madai kuwa amechoshwa na ahadi hewa za CCM kwa zaidi ya miaka 52 sasa.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati wa mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo uliofanyika katika Kijiji cha Ngonga, Kata ya Ngonga wilayani Kyela.
Mwalunga alisema ahadi zisizotekelezeka za CCM kwa muda wa miaka 52 zinachangia wananchi kuendelea kuwa maskini hivyo ni bora kuwe na mabadiliko ya chama tawala ili wananchi waweze kupata maendeleo ya kweli.
“Nimetafakari sana kuchukua maamuzi haya ya kujiunga na CHADEMA kwa kuwa ni chama ambacho kina dhamila ya kweli kusaidia wananchi na kutetea masilahi ya taifa kwa jumla,” alisema Mwalunga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bawacha wa Wilaya ya Kyela, Victoria Ipopo, alisema wananchi wanapaswa kutambua kuwa CHADEMA imejipanga kuwaelimisha wananchi kujua haki zao.
Alisema CCM imepitwa na wakati kwani haina tena fikra mpya za kuwasaidia wananchi wa hali ya chini bali imejipanga kuwanufaisha wenye pesa ambao ni vigogo wa juu wa chama.
Aidha, alisisitiza kuwa CHADEMA inaendelea na operesheni zake wilayani humo na kudai kuwa lengo ni kufanikisha kuwapata wanachama wapya katika kila kijiji na kuwa katika kata.

0 comments:
Post a Comment