Baraza la
madiwani lakataa kujadilitaarifa ya kamati ya fedha na mipango
Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Madiwani wa
Halimashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa
Katavi wamekataa kujadili taarifa ya kamati
ya fedha na mipango ya Halmashauri hiyo
iliyo wasilishwa kwenye kakao cha Baraza la madiwani kilichofanyika juzi kwenye
ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Mkoa wa Katavi
Baraza hilo la
madiwani lilikataa kupitisha taarifa hiyo kufuatia hoja imbalimbali
zilizotolewa na Madiwani ambao walidai kuwa taarifa hiyo iliyoletwa mbele ya
kikao hicho haikuwa imejitosheleza
Miongoni
mwakasoro zilizodaiwa kuwemo kwenye taarifa hiyo ni kutokuwemo kwa
viambata vinavyo onyesha namna ya mapato yandani yalivyo kusanywa na
sehemu yaliko toka
Diwani wa kwanza
kipinga taarifa hiyo kwenye kikao hicho cha Baraza la madiwani kilicho kuwa
kinaongozwa na makamu mwenyekiti wa Halimashauri ya mji wa Mpanda Yusuph Ngasa
alikuwa ni Diwani wa Kata ya Shanwe Abel Kapini
Diwani
Kapini alidai kuwa taarifa hiyo inamapungufu ambayo yatawafanya madiwani kama
wataamua kuijadili washindwe kuijadili
kitaalamu kwani haina mchanganuo
ambao utawawezesha madiwani kuhoji taarifa hiyo ya kamati ya fedha na
mipango
Kwa upande wake
diwani wa Kata ya Ilembo Wensilaus Kaputa
alilieleza Baraza hilo kuwa taarifa hiyo
haiko wazi kwani inaonekana taarifa zake zimfishwa kwa hari hiyo ni
vizuri irudishwe ikaandaliwe upya
Mwenyekiti wa
kikao cha baraza la madiwani baada ya kutolewa hoja hizo aliwashauri madiwani
wapige kura ili kujua ni madiwani
wangapi wanao unga mkono hoja hiyo ya kuikataa taarifa hiyo
Kufuatia uamuzi
wa mwenyekitimadiwani walipiga kura
ambapo kulikuwa na madiwani kumi kwenye kikao hicho na madiwani wanane waliunga mkono kuikataa
taarifa hiyo na madiwani wawili
waliikubali
Nae Mkugenzi wa
Halimashauri ya Mji wa Mpanda Selamani Lukanga alihaidi kuwa kikao kijacho cha
Baraza hilo watasomewa taarifa ikiwa na
viambatanisho na mchanganuo kama ambavyo walivyo hitaji madiwani
0 comments:
Post a Comment