KITUO
cha Televisheni cha Azam kimeahidi kuonyesha mechi za Yanga
zitakazochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na zile za
ugenini kwa sababu mkataba unawaruhusu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah amethibitisha kuwa Azam TV wapo huru
kuonyesha mechi yoyote ya Ligi Kuu Bara.
endelea.....................
endelea.....................
Habari nzuri ni kuwa ving’amuzi
vya Azam TV vitaanza kuuzwa mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya mwezi ujao
kabla ya mechi kuanza kuonyeshwa ama Oktoba 5 au Oktoba 9, mwaka huu.
Habari kutoka Azam TV zinasema
kuwa wataonyesha pia mechi zinazoihusu Yanga kwa sababu mkataba
unawataka kuonyesha mechi za Ligi Kuu Bara.
Yanga waligoma kusaini mkataba wa Azam TV kwa madai kuwa Sh 100 milioni ambazo kila klabu inapewa ni ndogo sana kwao.
“Mkataba wetu unasema kuwa
tunatakiwa kuonyesha mechi za Ligi Kuu Bara, kwa hiyo tutaonyesha pia
mechi za nyumbani na ugenini za Yanga, kwa sababu mkataba wetu tumesaini
na Kamati ya Ligi,” alisema mmoja ya viongozi wa Azam TV.
Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu wa TFF, Osiah alisema Azam TV wapo huru kuonyesha mechi yoyote kwa sababu mkataba unawaruhusu.
“Hata kama ni mechi za Yanga iwe Dar es Salaam au mikoani, Azam TV wanaruhusiwa kuonyesha,” alisema Osiah.
Katika hatua nyingine, wataalamu kutoka Afrika Kusini wanatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Azam TV mpaka Oktoba 15, mwaka huu.
“Hawa wataalamu wameomba kabla
hawajaondoka warushe mechi mbili laivu kuona kama kuna upungufu wowote.
Na ndiyo maana nadhani mechi za raundi ya saba za Oktoba 5 au mechi za
raundi ya nane za Oktoba 9, zitaanza kuonyeshwa moja kwa moja,” alisema
mmoja wa mabosi wa Azam TV.
Alisema wataanza kuonyesha mechi
za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mechi za mikoani zitaanza
kuonekana baada ya kuwasili kwa gari la OB Van ambalo litashughulika na
mechi za mikoani tu.
Kama
Azam TV itaanza kuonyesha mechi Oktoba 5, ina maana kwamba wataanza na
mechi ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting au siku inayofuata wanaweza
kuonyesha pia Yanga dhidi ya Mtibwa. Iwapo mechi hizo hazitaonyeshwa
maana yake mechi za raundi ya nane zinazoweza kuonyeshwa ni Azam dhidi
ya Mgambo Oktoba 9, au Simba dhidi ya Prisons Oktoba 12 na Ashanti dhidi
ya Coastal Union Oktoba 13.
Habari za ndani zinasema ving’amuzi vya Azam TV vitaanza kuuzwa wiki ya kwanza ya mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment