WANACHUO WAWILI WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA WATIA FORA KWENYE MATOKEO
Kwa kile ambacho kimeonekana ni tishio kwa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wanafunzi hawa kutoka kampasi ya Dodoma wameweza kupata ufaulu mkubwa katika masomo yao.
Bi. May Issa Mwanafunzi aliyehitimu shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa Manunuzi katika mahafali ya 49 ya chuo cha Elimu ya Biashara CBE Dodoma mwaka 2014 ametangazwa kuwa mwanafunzi wa kwanza aliyeongoza kwa ufaulu kwa kupata GPA ya 4.92. ambapo aliweza kupata alama A 28 , alama B+ tatu na alama B moja kati ya masomo 32 ya shahada yake ya kwanza ya Usimamizi wa manunuzi akifuatiwa na Bw. Peragius Cosmas aliyepata GPA ya 4.91.
Kwa upande wake Mwanafunzi mwingine Bw, Peragius Cosmas aliye kuwa akisoma Shahada ya kwanza ya Uhasibu yeye
pia
alionyesha maajabu kwa kuweza kupata GPA ya 4.91 ambapo aliweza kupata alama A 29 na alama B+ tatu kati ya masomo 32 ya shahada yake ya kwanza ya uhasibu.
Hivi karibuni katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) pia tulishuhudia Msichana Doreen Kabuche aki ]ongoza kwa ufaulu UDSM kwa kuwa Mhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, Doreen Kabuche alitangazwa kuwa kinara kwa ufaulu kwa kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima (Actuarial Science). Kwa alama hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano.
0 comments:
Post a Comment