TMF YAFADHILI MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NCHINI GHANA
Waandishi wa Habari wapatao tisa nchini Tanzania wamepata ufadhili kwenda nchini Ghana kwa ajili ya kupata mafunzo ambayo yatawajengea uwezo katika masuala ya utawala, uongozi, biashara, masoko pamoja na kuboresha maudhui katika vipindi vyao.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TMF, Ernest Sungura katika hafla ya kuwaaga wanahabari hao iliyofanyika Makao Upanga jijini Dar es salaam amesema TMF imekuwa ikiwawezesha wanahabari kupata mafunzo ya aina mbalimbali ndani na nje ya nchi. wanahabari hao wanakwenda nchini humo ambapo watapata mafunzo kwa siku 10 kuanzia Desemba 2 hadi 13 mwaka huu.
Akizungumzia waliochaguliwa Bw. Sungura amesema waliochaguliwa kwenda kupata mafunzo hayo ni baadhi ya wakuu wa vitengo kutoka vyombo vya habari, mameneja, wamiliki wa vyombo vya habari na maofisa masoko na mauzo pamoja na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio nchini Tanzania
0 comments:
Post a Comment