AL SHABAAB WAZIDI KUISHAMBULIA KENYA, WATU WENGINE 36 WAUAWA

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema kuwa watu 36 wameuawa katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya. Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo. Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, amesema wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya. Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera Kenya imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: