SIMBA YAGONGWA 1-0 NA KAGERA SUGAR

Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba na Kagera Sugar umemalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, na Simba kuambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera. Kagera Sugar ilipata bao lake kupitia kwa mshambuliaji wake Atupele Green katika dakika ya 21 kipindi cha kwanza na kufanikiwa kulinda ushindi huo hadi mwisho wa mchezo yaani dakika 90+6. Simba ambayo iliwachezesha nyota wake wote wageni akiwemo Dan pamoja na mdogo wake, Simon Sserunkuma, pia Nahodha wao Emanuel Okwi walijitahidi kusaka bao hata la kusawazisha lakini ngome ya Kagera Sugar ikawa imara kuhakikisha wanalinda bao lao ikiwezekana kuongeza linguine. Kutokana na matokeo hayo Simba inakuwa imebakia pale pale kwenye pointi 9 baada ya kucheza michezo 8, kutoa sare 6, kufungwa 1, pamoja na kushinda 1. Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho, ambapo vinara wa ligi kwa sasa Mtibwa Sugar watakuwa wakicheza na Stand United katika uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro, Tanzania Prisons na Coastal Union katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Huku, wakizi wa jiji la Dar wakishuhudia vita kati wanajeshi wa JKT Ruvu pamoja na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Chamazi majira ya saa 1:00 usiku.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: