KUHUSU SHINDANO LA MISS TANZANIA "KUPIGWA STOP" BAADA YA MADUDU KUTAWALA

i wish you happy chrismass and happy new year


Update_810_500_55_s_c1Tangu atangazwe aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu mengi yameongelewa kuhusiana na tetesi za udanganyifu wa umri na vitu vingine kadhaa vinavyomhusu mrembo huyo ikiwemo suala la umri wake na kiwango cha elimu yake ambapo yeye mwenyewe alikanusha taarifa hizo.


Story ikaendelea Novemba 8, 2014 siku ambayo Kamati ya Miss Tanzania ilikutana na waandishi wa habari Dar es salaam na kutangaza kwamba Sitti Mtemvu ameandika barua kwa hiari yake yeye mwenyewe, kwamba amelivua taji hilo hivyo kamati hiyo ikamtangaza Lilian Kamazima aliyekuwa mshindi wa pili kushikilia taji hilo.

Leo December 25 kuna taarifa kwamba Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.

Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.

Baada ya kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea arejee kwa nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa…“–Mngereza.

Shindano hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo.

Chanzo cha Habari: Gazeti la MtanzaniaDecember 25.
DSC07601
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: