MAJONZI: DALADALA YAGONGANA USO KWA USO NA LORI LA MAFUTA ARUSHA, ABIRIA WOTE WA DALADALA WAFARIKI DUNIA

Watu tisa wamefariki dunia na wawili kujeruhiwa vibaya katika ajali HIYO ya barabarani iliyotokea katika eneo Makumira wilayani Arumeru baada ya basi dogo aina ya Hiace kugongana uso kwa uso na lori la mafuta. Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amesema katika ajali hiyo imetokea majira ya saaa kumi jioni baada ya basi hilo dogo aina ya Nisan lenye namba za usajili T519dbv lililokuwa likitokea jijini Arusha kwenda Usariver kuhama kwenye saiti yake na kukutana uso kwa uso na Lori hilo la mafuta lenye namba za usajili T582 acr lilikuwa linatoka Moshi kwenda Arusha. Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi dogo na wameziomba mamlaka zinazohusika kuongeza adhabu kwa madereva wazembe. Mbunge wa Arumeru magharibi Mh Joshua Nassari amefika katika eneo la tukio kuungana na wananchi wengine kuokoa majeruhi na amependekeza kupanuliwa kwa barabara katika eneo hilo kama hatua ya kudhibiti ajali ambazi zimekithiri katika eneo hilo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: