DC LUDEWA AFANYA ZIARA KIJIJI CHA LUSALA NA ITUNDU, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Olivanus Thomasi akiambatana na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Festo Mkomba pamoja na wataalamu wa idara mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya hiyo ameendeleza ziara zake za kupita Kijiji kwa Kijiji kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Jana tarehe 02 - 05 - 2025 amefanya mikutano mikubwa ya hadhara katika Kijiji cha Lusala kata ya Lupanga na Kijiji cha Itundu kilichopo kata ya Mlangali ambapo alitoa nafasi kwa viongozi wa Chama, Kata, Vijiji na Wananchi kutoa kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi.
Mbali na kufanya mikutano ya Hadhara mkuu wa Wilaya huyo alipata fursa ya kutembelea zahanati ya Kijiji cha Lusala na Kituo cha afya Mlangali kwa lengo la kuona changamoto zinazoikabili ili kuweza kuzitatua.
Ikumbukwe kuwa ziara za kupita Kijiji kwa Kijiji kwa lengo la kufanya mikutano ya hadhara na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya wilaya ya Ludewa ni utaratibu aliojiwekea mkuu wa wilaya huyo kwa lengo la kutatua kero za wananchi.
#PUNGUZA_VIKAO_TUKUTANE SITE.See translation
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment