WILBARD MWINUKA ASHIRIKI MKUTANO NA WADAU WA RADIO BEST FM 90.3 LUDEWA NJOMBE TZ



Wakwanza kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Shule ya watoto Nicopolice Academy Bw, Agustino Mwinuka na wapili Kutoka kulia ni Mdau wa Maendeleo Mkoa wa Njombe Bw,Wilbard Mwinuka


Mkurugenzi wa Shirika la PADECO, Njombe Bw, Wilbard Mwinuka ambae ni Mwongoza Mada katika Mkutano wa wadau wa Radio Best fm Ludewa,

Meneja wa Kituo cha matangazo Radio Best Fm Bw, Nickson Mahundi akiendelea na Utaratibu ndani ya Ukumbi wa Mkutano,
Ni Baadhi ya Wadau wa Redio Best Fm Ludewa wakiendelea kusikiliza Mkutano,

































Uongozi wa Radio Best Fm 90.3 Ludewa Leo December 09/2017 Umeandaa na kufanya Mkutano Mkubwa na Wadau ambao ni Wasikilizaji wa Redio hiyo yenye makazi yake katika Mtaa wa Mkondachi eneo La Ludewa mjini Katika Mkoa wa Njombe, Kwa lengo la Kujadili na Kutoa Maoni Kuhusu mwenendo wa Kituo hicho cha Habari.

Mkutano huo unafayika katika Ukumbi wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ludewa ambapo Mwongozaji mkuu wa Mkutano huo katika Mada husika ni Mkurugenzi wa shirika La PADECO Njombe, Bw, Wilbard Mwinuka akisaidiana na Mkurugenzi wa Shule ya Watoto wadogo inayoendelea na Huduma kwa watoto katika wilaya nzima ya Ludewa na Mkoa wa Njombe bw, Agustino Mwinuka pamoja na Meneja wa Kituo cha Redio BEST FM Bw, Nickson Mahundi.

Majadiliano Makubwa katika mkutano Huo yanalenga namna ya kuboresha Redio hiyo pamoja na Wafanyakazi wake hasa kipindi hiki cha kufunga mwaka 2017 ili ifikapo January mwaka 2018 Kituo hicho kiweze kusimama Vyema katika Utendaji wake wa Kazi.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Huo na Wadau pamoja na Viongozi mbalimbali Waliofika katika mkutano wakitokea Ludewa, Njombe pamoja na Mikoa Jirani ya Ruvuma, Mbeya na Songwe Afisa Utamaduni wilaya ya Ludewa bw, Joseph Mvanga anaesimamia Maswala ya Utamaduni pamoja na Habari wilayani Ludewa Amekipongeza Kituo hicho kwa Kuandaa mkutano Huo mkubwa wenye Lengo la Kuboresha Utendaji kazi na Ubora katika Sekta Hiyo ya Habari.

Edelea kuwa nasi www.maikoluoga.blogspot.com Tutakuletea Taarifa kamili kwa yanayoendelea sasa kwenye mkutano huo wa wadau wa Redio Best Fm Ludewa. 







Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: