wakosoa uchaguzi mdogo Tanzania






Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini Tanzania kimesema uchaguzi mdogo wa marudio wa madiwani kwenye kata 43 uliyofanyika Novemba 26, 2017 ulikuwa na uvunjifu wa haki za binadamu.
Wakili Anna Henga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, amesema pamoja na mambo mengine kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu zinazo simamia uchaguzi huo ulionyesha ushindani mkali wakati wa kampeni.
LHRC imesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa licha ya kuwa uchaguzi umefanyika kwa uhuru na haki katika baadhi ya kata, katika maeneo mengine kumekuwepo na vitendo vya matumizi mabaya ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa na vitendo vya kuwatia hofi wapiga kura.
LHRC imeitaka serikali kuchukulia hitilafu katika chaguzi ndogo kama hizi za udiwani kwa uzito wa kipekee ili kuepuka athari za namna hii katika chaguzi kubwa zijazo.
Uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata 43 zilizopo kwenye mikoa 19 Tanzania, ulifanyika ili kujaza nafasi zilizowazi katika kata hizo baada ya madiwani waliokuwepo kufariki, kujiuzulu na wengine mahakama kutengua uwakilishi wao.
Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa maeneo yaliyoripotiwa kukumbwa na vurugu wakati wa uchaguzi, mengi yako Mkoa wa Arusha, hali ambayo ilifanya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwataka wagombea wake wa udiwani katika kata zote za Wilaya ya Arumeru kujitoa.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema Chadema kilijitoa kwenye uchaguzi wa kata tano za jimbo la Arumeru Mashariki.
Mbowe alidai uchaguzi huo wa marudio ulikuwa na matukio ya ukikukaji sheria ikiwa ni pamoja na mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: