Dr. Seuri Mollel akithibitisha kutokea kwa tukio hilo |
Miongoni mwa wahanga watukio hilo la Radi akiwa amelazwa katika hospital ya wilaya ya Ludewa |
Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilya ya Ludewa Mh, Edward Haule alipowatembelea wahanga waliolazwa katika hospital ya Wilaya ya Ludewa |
Katibu wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Ludewa Akizungumza nje ya Hospital ya wilaya ya Ludewa baada ya kuwatembelea wahanga wa Tukio la Radi, |
Na Maiko Luoga Ludewa,
Wakati Mvua kubwa zikiendelea kunyesha kwakuambatana na Radi Hapo jana December 2 mwaka huu 2017 wilayani Ludewa Mkoani Njombe Mvua hiyo inaripotiwa kusababisha Ajali ya Radi katika Kambi ya Akina Mama wajawazito Eneo la Mwembeni Ludewa Mjini.
Akina Mama 11 walipigwa na Radi katika eneo hilo la mwembeni ambapo ni Kituo cha Akina mama wajawazito wanaosubiri muda wao wa kujifugua ufike ili waweze kuhudumiwa katika Hospital ya Wilaya ya Ludewa ambapo ajali hiyo ya Radi ilihusisha wauguzi wa wajawazito hao ambao idadi yao hadi jana Usiku ilikuwa 10 pamoja na Mama mmoja ambae ni Mjamzito na kufanya idadi yao kufika 11.
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo la Ajali ya Radi kaimu mganga mkuu wa Hospital ya wilaya ya Ludewa Dr. Seuri Mollel Alisema kuwa Ajali hiyo ilitokea Jana majira ya saa 11 Jioni wakati Mvua kubwa ikiendelea kunyesha na kusababisha Akina Mama 11 Kujeruhiwa wakiwa Ndani ya vyumba vyao ambapo kati ya hao Akina mama wawili walipata maumivu makali Huku akisema kuwa wakati mvua inaendelea kunyesha Wahanga hao walikuwa ndani ya vyumba vyao lakini hawakufunga madirisha huku baadhi yao wakifanya mawasiliano ya Simu ghafla Wakakutwa na tukio hilo la Radi.
Dr.Morel Aliongeza kuwa Wagonjwa wawili ndio walioumia zaidi lakini wengine Tisa walipata majeraha ya kawaida katika sehemu mbalimbali za miili yao ikiemo miguuni na Mgongoni pamoja na
Huyo Mama Mjamzito ambae baada ya vipimo ameonekana kuwa anaendelea vizuri yeye pamoja na Mwanae aliyeko tumboni.
Aidha Mganga huyo amewataja Wahanga hao waliopatwa na Ajali hiyo ya Kupigwa na Radi kuwa ni pamoja na Nuruh Haule aliyetokea kijiji cha Ibumi, Teresia Nkwera,Ronika Haule na Elgia Lukuwi waliotokea Nkomang'ombe Pamoja na Riziki Mdanga mkazi wa Kijiji cha Ludewa K,
Wengine ni Veronika Haule wa Kijiji cha Lihagule,Asumta Haule kutoka Kijiji cha Kipangara,Selina Ngailo Kutoka Makonde,Kondrad Lugome Kutoka kijiji cha Muholo,Lusekele Muhagama Kutoka Kimelembe,Pamoja na Mama Mjamzito aliyefahamika kwa jina la Veronika Ngalawa Kutoka katika kijiji cha Kipangara Wilayani Ludewa.
Licha ya Kuihakikishia jamii ya Ludewa Kuwa Wagonjwa hao watarudi katika hali zao za kawaida Dr. Morel pia Alitoa wito kwa Akina Mama Wajawazito pamoja na Wauguzi wao wanaoishi katika kambi ya wajawazito Eneo la Mwembeni Ludewa Mjini kuwa makini wakati mvua zikiendelea kunyesha na kuachana na tabia ya kutumia simu kwakuwa Radi haizuiliki na Maranyingi hufuata Mikusanyiko ya Watu wengi.
Mapema leo Asubuhi Akizungumza na Mwandishi wetu kwa Njia ya Simu kaimu Mganga mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Ludewa Dr.Mollel Alisema kuwa wagonjwa wote 11 wanaendelea vizuri huku akithibitisha kuwa licha ya Tukio hilo pia siku chache zilizopita Katika Kijiji cha Luana Wilayani Ludewa Mtu Mmoja alifariki dunia na wengine watatuwalipata Majeraha na kutibiwa katika Hospital ya Wilaya ya Ludewa Kutokana na Ajali ya Radi.
Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mh, Edward Haule na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ludewa Mh, Bakari Mfaume kwapamoja walifika katika eneo la Tukio na kushuhudia wahanga wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya kutokana na Tukio la Ajali walilokutana nalo kisha wakatoa pole kwa wahanga hao.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment