Miongoni mwa maneno yaliyokwenye sabuni za kunawia ukeni. |
Miongoni mwa mambo hayo ni matumizi ya madawa mbalimbali ikiwemo yake ya kuongeza hips, makalio, kubadilisha rangi ya ngozi na hata kufanyia operesheni sura ili kuwa na muonekano ambao wanauona bora zaidi.
Pia kumekuwa na aina mbalimbali za sabuni kutoka ndani na nje ya nchi ambazo zimekuwa zikiuzwa ambazo zinadaiwa hurejesha ubikira zimesambaa sana madukani huku wateja wakubwa wakiwa ni wasichna na wanawake.
Hata hivyo walaatalam mbalimbali wanasema kuwa sabuni hhizo ambazo hutummika kwa kunawia sehemu za siti husaidia kurudisha bikira kwa mwanamke na hata kuwa na mnato.
Lakini wanaootumia sabuni hizo wameonywa kuwa sabuni hizo zina kemikali zenye madhara makubwa kwa mtumiaji kwani zina uwezo mkubwa wa kusababisha kansa ya shingo ya kizazi.
Kwa mujibu wa Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka anasema hivi sasa kumekuwa na sabuni mbalimbali ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho si kweli.
Mtaalam huyo Anasema Sabuni hizo zinapunguza tu majimaji yaliyo sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume kupata ugumu kwenye muingiliano kwa vile mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa.
Pia michubuko inapotokea ni rahisi mwanamke kuambukizwa magonjwa ya zinaa hata virusi vya Ukimwi. Sabuni hizo zinatengeneza hali fulani ukeni lakini haiwezi kurejesha hali ya maumbile iliyopotea.
Mfamasia huyo anasema wanaotumia sabuni hizo wako katika hatari kubwa ya kuambukuzwa magonjwa na hata kupata saratanni ya shingo a usazi kwani kemikali zinazotumika katika kutengeneza sabuni hizo zina athari kubwa kiafya.
Anataka wanawake kutatambua thamani yao na kuachana na matumizi ya sabuni hizo ambazo hazina manufaa yoyote na badala yake zimekuwa na madhara makubwa kwao.
Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kanda ya Dodoma, Fredrick Luyangi anasema mrudiano wa athari hasa kwa matumizi ya sabuni huleta athari kubwa mwilini na wakati mwingine kutengeneza kansa taratibu bila mhusika kufahamu.Sabuni hizo husababisha kansa ya kizazi na kubainisha sabuni hizo licha kupigwa marufuku zimekuwa zikiuzwa kwenye maduka ya vipodozi.
“Mara nyingi kwenye operesheni zinazofanyika zimekuwa zikiondolewa sokoni lakini hata hivyo zimekuwa zikiingizwa kwa wingi hali inayofanya zoezi la kudhibiti kuwa gumu” anasema.
Anawataka wanawake kuacha matumizi ya sabuni hizo ambazo zina madhara makubwa sana kwao kwani zikikosa wanunuzi zitaondoka sokoni.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment