CAF yatangaza ratiba ya michuano ya klabu barani Afrika



Shirikisho la Soka barani Afrika limetangaza ratiba ya michuano ya klabu bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho msimu wa mwaka 2018 huku wawakilishi wa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati wakijua wapinzani wao.
Mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya klabu katika bara la Afrika hushirikisha timu zilizofanya vizuri katika Ligi za mataifa mbalimbali na yanatarajiwa kuanza Februari mwaka ujao.
Katika hatua za awali kwa upande wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika, mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia watapambana na klabu ya Leones Vegetarianos kutoka Guinea ya Ikweta huku mabingwa wa soka nchini Uganda KCCA wao wataanzaia ugenini nchini Madagascar kwa kucheza na CNAPS Sports.
Yanga ya Tanzania itaanza kampeni yake kwa kucheza na ST. Louis ya Ushelisheli.
Rayon Sports ya Rwanda yenyewe itaanzia nyumbani kwa kuchuana na LLB Academic ya Burundi wakati AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo itaipokea Mighty Wonderers ya Malawi.
Wawakilishi wa Zanzibar katika ligi ya mabingwa JKU watachuana na mabingwa wa soka nchini Zambia, Zesco United, nayo Saint Gorges ya Ethiopia itaonyeshana kazi na Wahu Salamu ya Sudan Kusini.
KOMBE LA SHIRIKISHO
APR ya Rwanda itachuana na Anse RĂ©union kiutoka Shelisheli huku Simba ya Tanzania yenyewe itachuana na Gendamarie ya Djibout. Zimamoto ya Zanzibar itachuana na wawakilishi wa Ethiopia Welatya Dicha wakati AFC Leopards ya Kenya itakipiga na Fosa Junior ya Madagascar.
Mechi nyingine itazikutanisha Olympic Star ya Burundi ambayo itachuana na Etolie Filante ya Burkinafaso.
Michuano ya ngazi ya klabu barani Afrika mwakani yataanza mwezi Februari na kutamatika Novemba au Disemba 2018.







Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: