Binti afanyiwa upasuaji 50 alingane na mcheza filamu Angelina Jolly


Sahar aliyefanyiwa upasuaji 50 ili afanane na Angelina Jolly
Mara kadhaa tumekuwa tukisikia simulizi za kuhusu mashabiki  ambao hubeba mapenzi yao kwa watu maarufu kwa kupitiliza, yaani mahaba yaliyopitiliza kiasi cha kutaka wafanane nao.
Hayo yamemtokea binti mdogo wa nchini Iran, Sahar Tabar ambaye amepata umaarufu hivi karibuni kutokana na sababu hii muhimu.
Binti huyu wa miaka 19,  ambaye kwa sasa anawafuasi takribani 400,000 katika ukurasa wake wa Instagram, amepitia upasuaji baada ya upasuaji mradi tu aonekane kama mchezaji wa filamu nyota wa Hollywood, Angelina Jolie ambaye anampenda zaidi.
Amefanyiwa upasuaji wa sura yake kwa takribani mara 50  ili aonekane kama mwanamama huyo wa kimarekani na nyota wa filamu za ‘action’.
Anasema mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo, alitakiwa kufuata masharti ya chakula ili aweze kupunguza uzito kwa lengo la kufikia umbo la Angelina mwenye mwili mwembamba pia.  


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: