WASTAAFU LUDEWA, WAASWA KUTOPELEKA MAFAO YAO YA UZEENI KWENYE POMBE



 
Afisa Elimu Kata ya Ludewa Mwalimu Lenis Mtitu Mwenye Koti Jeusi akisalimiana na Baadhi ya walimu waliojitokeza katika Hafla ya Kuwaaga walimu wenzao.
Ni walimu Wastaafu 2017 kata ya Ludewa wakiwasili Ukumbini Ludewa Mjini,

Walimu Wastaafu Wakiwa Meza kuu Tayari kwakuendelea na Sherehe ya Kuagwa,
Baadhi wa Walimu na Wageni waalikwa Wakiserebuka Ukumbini kwa Burudani ya Muziki wakati wa Kuwaaga Walimu wenzao Ambao wanastaafu Leo,
Mwenyekiti wa Sherehe Mwalimu Lenisi Mtitu Ambae ni Mratibu Elimu Kata ya Ludewa Akizungumza jambo mbele ya Walimu wastaafu pamoja na Wageni Waalikwa,
Walimu wa Shule ya Sekondari Chief Kidulile Wakiongozwa na Mwalimu Wille Mwenye koti la Bruu na Karatasi Mkononi pamoja wakiimba Shairi lenye ujumbe mzito kwa Wastaafu hao.
Nisehemu ya Walimu wa Shule ya Sekondari Chief Kidulile Ludewa Mjini.

Na Maiko Luoga Ludewa 
Ustawi wa walimu Kata ya Ludewa mkoani Njombe siku ya leo November 29 mwaka 2017 kwaumoja wao wanawaaga walimu saba waliostaafu mwaka huu 2017 waliokuwa wanafanya kazi katika kata ya Ludewa wilayani Ludewa.

Hafla hiyo ndogo ya kuwaaga walimu hao saba inaendelea muda huu katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa ikihudhuriwa na walimu wenzao wa shule za msingi na Sekondari ndani ya Kata ya Ludewa pamoja na Wageni mbalimbali walioalikwa wakiwemo baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa pamoja na Diwani Wa kata ya Ludewa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri Bi, Monica Mchilo.

Mwenyekiti wa Sherehe hiyo ni Mratibu elimu kata ya Ludewa Mwalimu Lenis Mtitu Na Sherehe hiyo Imetawaliwa na Ujumbe pamoja na Ushauri kwa wastaafu hao kuwa wakawe picha nzuri kwa jamii pamoja na kutumia vyema Pesa watakayolipwa na Serikali kama kiinua mgongo baada ya Kufanya kazi kwa Muda wote wakiwa Kazini.

Haya hapa Majina ya Walimu wastaafu Saba 2017 katika kata ya Ludewa 
  1. CATHERIN MHAGAMA Alianza kazi tangu July1979 na Kustaafu kazi ni July 2017 akiwa na Umri wa Miaka 38 Kazini.
  2. RESTITUTA MBENA  Alianza kazi tangu July1977 na Kustaafu kazi ni June 2017 akiwa na Umri wa Miaka 36 Kazini.
  3. JOHN MAPUNDA  Alianza kazi tangu July1984 na Kustaafu kazi ni December 2017 akiwa na Umri wa Miaka 33 Kazini
  4. DEODATHA HAULE  Alianza kazi tangu July1981 na Kustaafu kazi ni September 2017 akiwa na Umri wa Miaka 36 Kazini.
  5. PHILOMENA MGAYA  Alianza kazi tangu July1981 na Kustaafu kazi ni July 2017 akiwa na Umri wa Miaka 36 Kazini.
  6. ZIPORAH MHAGAMA  Alianza kazi tangu July1980 na Kustaafu kazi ni October 2017 akiwa na Umri wa Miaka 37 Kazini.
  7. ANNA BANGE  Alianza kazi tangu July1981na Kustaafu kazi ni September 2017 akiwa na Umri wa Miaka 36 Kazini.





Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: