Mwanadada huyo alijikuta akifunua chupi yake kwa kaka huyo anayeuza njegere kutokana na ubize wa mume wake uliosababishwa na shughuli zake za kibiashara ambazo humfanya mara nyingi awe nje ya nchi na kushindwa kupata muda wa kutosha kukaa mke wake.
Tangu Mrembo huyo afunge ndoa na mumewe mwaka 2010 alieleza kuwa hajawahi kukaa na mumewe wiki moja nzima kwani mume wake huja na kuondoka kwa muda mfupi sana na apomwambia kuhusu kukaa muda mrefu Mume huyo hudai kuwa biashara zake zinaweza kutetereka hivyo zinahitaji usimamizi wa karibu kutoka kwake.
Ndipo katika harakati za kuondoa upweke huo na kutuliza hamu yake kimapenzi alijikuta akiingia mikononi mwa kijana mmoja muuza njegere aliyekutananae siku moja mwanadada huyo alipokuwa anatoka na gari yake nje ya geti la nyumba yake na aliposhindwa kuzuia hisia zake ni pale alipoweka gari pembeni na kumwomba kijana huyo aingie ndani ya nyumba ili ampimie njegere.
Dada huyo alijikuta akimsimulia kaka huyo habari ya ubize wa mumewe na kumwomba kaka huyo ampe raha kwa kumpa penzi pale atakapokuwa anahisi kuzidiwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Kaka huyo alijikuta ameingia majaribuni kwa kumkubalia dada huyo jamboambalo lilizua gumzo kwa marafiki na majirani waliposhtukia suala hilo kutokana na kushamiri kwa penzi la wawili hao huku Mume akiwa hana hili wala lile
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment