Unapokuwa umempata mpenzi mpya lazima utafute muda wa kuzungumza naye mambo ya msingi yanayokuhusu wewe kwa mfano tabia za ndani ulizonazo,mambo unayyapenda nk.hapo utakuwa mtu mwenye kujiamini sana katika uhusiano wenu.Mweleze mambo yafuatayo:-
MWELEZE MAMBO UNAYOYAPENDA
Kujua uwezo wako na sifa zako nzuri kutafanya ujiamini zaidi. Kila mmoja wetu ana vipawa mbalimbali. Kwa mfano, watu fulani wana kipawa katika uchoraji au muziki, ilhali wengine wana uwezo mzuri katika michezo au wengine wanauwezo mkubwa sana darasani. Ikiwa ni vigumu kwako kutaja sifa uliyo nayo kwa wasiwasi labda utaonekana unajisifia waweza kumwambia mpenzi wako kwamfano,mimi napenda sana kuimba badala ya kumwambia mimi najua sana kuimba.
MWELEZE KUHUSU UDHAIFU WAKO
Hili ni jambo la msingi sana kwa wapenzi kufahamiana tangu siku za mwanzo,kufahamu mapema udhaifu wa mpenzi wako kunasaidia kulinda makosa utakayomfanyia ambayo yamesababishwa na udhaifu wako na kwamba halikuwa kusudio lako.Hata kama unapenda sana ngono we usione aibu mwambie kwa sababu kweli ni kitu unachokizimia kupita kiasi, usiposema ukweli ni tatizo kwani itafika wakati unaogopa kusema kwamba unanyege eti kisa atakufikiria vibaya kwa sababu jana tu ulifanya nae,matokeo yake unaanza kuwaza kuwa na mtu mwingine wa pembeni jambo ambalo si sahihi.
UWEZO WAKO KIUCHUMI
Lazima mwanzoni kabisa wa mapenzi yenu mpenzi wako afahamu uwezo ulionao kiuchumi,kama unafanya kazi basi kazi gani ili suala la kipato chako liwe wazi ili kuepuka kukubebesha majukumu yaliyo nje ya uwezo wako.Kudanganya kwamba unapesa za kutosha na kazi nzuri sio jambo la busara kwani mpenzi wako atakubebesha majukum akitambua kuwa wewe ni mtu mwenye pesa na kazi nzuri sasa kama ulidanganya kumbe wewe ni kapuku utakoma, mwenzio anataka umtoe out kila weekend,mara anataka Samsung galaxy nk.utakuwa na wakati mgumu sana.
MSIMAMO WAKO MAISHANI
Suala la kitu gani unakipa sana kipaumbele ni muhimu mpenzi wako afahamu kwani asipofahamu itakuwa rahisi sana kukukwaza na kujikuta akiambulia kupigwa hata makofi kumbe hafahamu wewe ni kitu gani hasa unathamini katika maisha yako,kuna watu kipaumbele chao ni wazazi kwamba ni bora umkorofishe yeye kuliko wazazi wake hivyo ni vizuri sana mpenzi wako akitambua mambo ya msingi kuhusu wewe na hakuna mwingine wa kumwambia bali ni wewe mwenyewe,ukifanikisha hili mapenzi yenu yatadumu kwa muda mrefu na mtaishi kwa furaha daima.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment