WALIOJIUDHURU MKONGOBAKI WAKUBALI KUREJEA KAZINI,LUDEWA


Kulia aliyevaa Head Phone ni Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bw,Bakari Mfaume akiwa na Mwenyekiti wa UV,CCM wilaya ya Ludewa Bi, Theopister Mhagama katika Studio za Redio Best Fm Ludewa.
                     Na Maiko Luoga Ludewa,
Akizungumza leo November 23 katika kipindi cha Nuru ya Asubuhi Cha Redio Best Fm Ludewa majira ya Saa mbili kamili Asubuhi Katibu wa chama cha Mapinduzi ccm wilaya ya Ludewa Bw, Bakari Mfaume Alithibitisha hilo na kusema kuwa sasa shule hiyo ya Sekondari ya Kata ya Mkongobaki Itajengwa katika eneo La Nyaudole ambapo Awali baadhi ya wananchi wa Kata ya Mkongobaki wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe walikuwa wanapinga Shule hiyo kujengwa Nyaudole wakitaka ijengwe katika kijiji cha Ugela ambapo ni Makao makuu ya kata ya Mkongobaki.

Alisema kuwa Mgogoro huo juu ya wapi ijengwe shule ya Sekondari ya kata ya Mkongobaki kati ya maeneo Manne yaliyopendekezwa Awali ulisababisha baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji cha Ugera na Lipangara wakiwemo wenyeviti wa Vijiji hivyo viwili na wenyeviti wao wa Vitongoji kuandika Barua za kujiudhuru wakidai kuwa wananchi wao hawawezi kwenda kujenga shule hiyo katika Eneo la Nyaudole.

Kufuatia Mgogoro huo Uongozi wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Ludewa Ukiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho wilaya ya Ludewa Mh, Stanley Kolimba pamoja na katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bw, Bakari Mfaume jana November 22 ulifanya ziara katika kata ya Mkongobaki na kuzungumza na Uongozi pamoja na wananchi wa Kata hiyo juu ya kutafuta mwafaka wa Ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari ya Kata ya Mkongobaki.

Alipohojiwa na Watangazaji wa kipindi cha Nuru ya Asubuhi cha Redio Best Fm kama mgogoro huo Umeisha na Vipi kuhusu viongozi waliojiudhuru, Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa alisema kuwa Mgogoro huo Umefikia mwafaka baada ya Mazungumzo kati ya Uongozi wa ccm wilaya ya Ludewa na Viongozi waliojiudhuru, Diwani wa Kata ya Mkongobaki pamoja na wazee washauri wa Kata ya Mkongobaki ambao kwapamoja wamekubaliana kuanza Ujenzi wa shule hiyo katika Kijiji cha Mkongobaki, katika eneo la Nyaudole.

"Nikweli Ndugu mtangazaji lazima ni kubali kuwa mwanzoni kulikuwa na maelewano mabovu kati ya viongozi na wananchi wale wa kata Mkongobaki ila tulipofika Pale jana Mkongobaki tuliwaelimisha kuwa shule itakayojengwa ni yakata ya Mkongobaki hata ingejengwa kwenye kijiji chochote ndani ya Kata hiyo bado ingeitwa Shule ya kata ya Mkongobaki kwahiyo hakuna haja ya kila mtu kutaka shule ijengwe katika Kijiji chake". Alisema katibu huyo wa ccm Wilaya ya Ludewa Bw, Bakari Mfaume.

Ikumbukwe kuwa kabla ya viongozi hao kutembelea katika kata ya Mkongobaki Mgogoro huo Ulifika katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh, Andrea Tsere aliyetoa uamuzi kuwa Shule inatakiwa Ijengwe Nyaudole kwa mujibu wa Utafiti wa timu ya Wataalamu aliyoiunda na kudai kuwa Maeneo mengine yaliyopendekezwa hayakukidhi vigezo vilivyopangwa.

Licha ya kuwa eneo la Nyaudole linaukubwa wa Ekari 75 pia huduma nyingine kama maji, Umeme na Barabara zipo jirani tofauti na maeneo mengine yasiyozidi ekari 15 lakini bado Mgogoro huo ulikuwa na Mvutano mkubwa kila mwananchi akitaka Shule ijengwe katika kijiji chake hadi kusababisha Baadhi ya Viongozi wa Serikali ya kijiji cha Ugera na Lipangara kujiudhuru Pamoja na wenyeviti wao wa Vitongoji kwa madai kuwa hawataki shule ya sekondari Ijengwe Nyaudole wakidai kuwa eneo hilo liko mbali na vijiji vya Ugera na Lipangara.

Baada ya Usuluhishi huo wa jana hatimae viongozi waliojiudhuru nafasi zao wamekubari Kurejea madarakani ikiwa ni pamoja na  kuondoa barua zao za Kujiudhuru tayari kwakuendelea na Ujenzi wa Shule hiyo ya Sekondari katika Eneo la Nyaudole katika kijiji cha Mkongobaki hivyo wananchi wa Vijiji vya Ugera na Lipangara wataenda kufanya shuhuli za maendeleo ya ujenzi wa Shule hiyo katika Eneo la Nyaudole




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: