(Katikati) kaimu katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao akizungumza na waandishi wa habari
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao leo Alhamisi, amekanusha tuhuma za wajumbe wa kamati kuu wa shirikisho hilo la mpira nchini kujilipa mamilioni ya fedha na kusema kuwa tuhuma hizo ni uzushi na zinalengo la kuwachafua.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, leo Kidao amesema, tangu uongozi mpya chini ya rais Wallace Karia uingie madarakani, chombo hicho kimejitahidi kuhakikisha wanaondoa makandokando na kero hususan katika malipo na suala la rushwa hivyo madai hayo siyo ya kweli.
Kaimu Katibu huyo amesema, suala la nyongeza ya posho halijawahi kuzungumziwa kabisa, licha ya kujitokeza na kuleta mvutano.
"...Ndio kulikuwa na mjadala mkubwa juu ya posho ya kujikimu ya rais na makamu wake. Rais aligoma kupewa posho na kuandaa waraka wa kwanini hataki na amesisitiza mapato yote ya TFF yaende kwenye mpira moja kwa moja," Kidao.
Aidha Kidao amesema, kama TFF hawazui wala kukataa kukosolewa kwa nia njema ya kujenga ila wametambua kuwepo kwa baadhi ya wenye nia mbaya na uongozi uliopo ambao wanazua uvumi wa kuwachafua jambo ambalo hawatalikalia kimya.
"Tayari tuna majina 10 ya watu ambao walikuwa wanasambaza taarifa hizi za uongo na kutuchafua kinyume kabisa na Sheria ya Mitandao. Tunataka wakathibitishe tuhuma hizi kwenye vyombo vya dola," Kidao.
Amesema, mwanasheria wa TFF anakwenda kushughulikia suala hilo licha ya kwamba uamuzi huo utawachukiza wengi na kuwaumizi wengine na kuwakumbusha wanahabari kufuata sheria na kanuni huku akisisitiza kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment