Mzazi amkata mwanaye sehemu za siri ili kuondoa nuksi ya umasikini






Mzazi mmoja nchini India amekamatwa na polisi kwa kosa la kumkata mwanaye wa kiume sehemu za siri kwa imani ya kuondoa mikosi kwenye familia yake.
Mtuhumiwa wa mauaji, Ram Gopal Patel katikati kwenye picha.
Mwanaume huyo, Ram Gopal Patel, 39 amemuua kwa kumkata kwa shoka mwanaye aitwaye Rupesh (13), baada ya kupewa maelekezo na mganga wa kienyeji kuwa ili afanikiwe ni lazima amtoe mwanaye kafara kuondoa mikosi.
Mganga wa kienyeji, Rajesh Yadav .
Wakati na mahojiano na polisi juzi (Tarehe 7 Novemba 2017) mjini Baloda Bazaar, Bw. Patel amekiri kufanya tukio hilo na kusema kuwa alishirikiana na Mganga huyo wa kienyeji aitwaye Rajesh Yadav (19) kushika mtoto wake kisha kumkata uume.
Mama mzazi wa mtoto huyo aitwaye Sunita (35) amesema siku ya tukio alienda kazini lakini aliporudi jioni alimkuta mumewe akiwa amelowa damu huku mtoto wake akiwa amelala sebuleni.
Tunawashikilia Ram Gopal Patel ambaye ni mzazi wa Rupesh na Rajesh Yadav ambaye ni mganga wa kienyeji kwa kosa la tuhuma za mauaji. Watuhumiwa wote wawili wamekiri kutekeleza mauaji hayo ambapo wamesema kuwa siku ya Jumamosi (Tarehe 25 Novemba 2017) wakiwa na shoka walimpiga na shoka kichwani mtoto aitwaye Rapesh na kisha kumkata uume. Leo (jumatatu) tunawapeleka mahakamani.“amesema Kamanda wa Polisi mjini Baloda Bazaar, Ram Gopal Soni.
Kwa mujibu wa gazeti la Hindustan Times la nchini India limeelezwa kuwa watoto wengi wa kiume wa kwanza kuzaliwa kwenye familia mjini Baloda Bazar hupotea kwenye mazingira tatanishi kutokana na imani za kishirikina kuwa watoto hao huwa wanakuwa na mikosi.
Chanzo : Daily Mail



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: