MWANDISHI MMAREKANI AKAMATWA, ADAIWA KUMTUSI RAIS MUGABE



Rais Robert Mugabe akihutubia mkutano jijini Harare, Zimbabwe, Novemba 8 mwaka huu.
Mmarekani, Martha O’Donovan akifikishwa Mahakama ya Harare, Novemba 4 mwaka huu.

MWANDISHI wa Marekani, Martha O’Dovovan, hivi majuzi alikamatwa na kufikishwa mahakamani mwanzoni mwa mwezi huu nchini Zimbabwe kwa kosa la kumwita Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo “mchoyo na mtu mgonjwa”.

O’Donovan ambaye aliachiwa kwa dhamana, anakabiliwa na kifungo kisichofikia miaka 20 jela akipatikana na hatia.

Mwandishi huyo ambaye alikana kosa hilo alilodaiwa kuliandika kwenye mtandao wa Twitter, alikabidhi pasipoti yake mahakamani na anatakiwa kuripoti polisi mara mbili kwa wiki wakati kesi yake iliyoahirishwa itakaposikilizwa mahakamani.

Mahakamani, mwandishi huyo alisema madai hayo ya kumtukana rais huyo mwenye umri wa miaka 93, hayana msingi na yana lengo la kumchafua.

Kukamatwa kwa mwandishi huyo kunafanyika mara ya kwanza tangu Mugabe ateue rais wa masuala ya mtandao mwezi mmoja uliopita, jambo ambalo lilishutumiwa na wanaharakati kwamba lilikuwa limelengwa kwa vyombo vya habari.
O’Donovan amekuwa akifanya kazi na televisheni ya Magamba ya nchini humo ambayo huelezea vipindi vyake kuwa ni vya burudani na kuchekesha.




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: