Makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke aliyemtembelea ofisini kwake Ikulu, Dar es Salaam
Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan leo,Alhamisi amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi kutoka nchi nne kwa nyakati tofauti ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais alianza kukutana na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ambapo makamu wa rais aliupongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili na kusema Uingereza imekuwa ikiifadhili Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini alielezea kuridhishwa kwake na kasi ya uwekezaji kutoka Uingereza na kuelezea kwamba nia ya Uingereza ni kuongeza uwekezaji .
Makamu wa rais alimhakikishia balozi wa Uingereza kuwa milango ipo wazi kuja kuwekeza kwa wawekezaji wa Uingereza na katika kuelekea Tanzania ya Viwanda mazingira ya uwekezaji yataboreshwa zaidi ili wawekezaji waje kwa wingi zaidi Tanzania.
Mara baada ya mazungumzo na Balozi wa Uingereza makamu wa rais alikutana na Balozi wa Canada nchini, Ian Myles ambapo makamu wa rais pamoja na mambo mengine alizungumzia azma kubwa ya Tanzania ni kuona vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua vinapungua ama kumalizika kabisa pia alimueleza Balozi huyo kuwa wanawake wamedhihirisha wakipewa nafasi katika uongozi wa kijamii ama wa kisiasa wanaweza kuongoza," wanawake sasa wamekuwa kwenye vikosi vya kulinda amani." Makamu wa rais.
Balozi wa Canada alimpongeza makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu nchini ambapo pia alisisitiza kudumishwa kwa mahusiano na ushirikiano ulioanzishwa miaka 56 iliyopita.
Wakati huo huo makamu wa rais, alikutana na Balozi mpya wa China nchini Tanzania, Wang Ke ambapo makamu wa rais aliishukuru serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa jitihada zake za kusaidia maendeleo na kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo, makamu wa rais alisema ushirikiano kati ya nchi mbili hizi umezidi kuimarika tangu kuanzishwa na waasisi wa mataifa haya.
Aidha makamu wa rais alimpongeza Rais wa China, Xi Jing Ping kupitia kwa Balozi Wang Ke kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).
Balozi wa China nchini alimpongeza makamu wa rais kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendelea kudumisha mahusiano na kufanya kazi vizuri.
Pia Makamu wa Rais alikutana na Balozi wa Oman, Ali Al Mahruqinchi ambapo walifanya mazungumzo ya kawaida ambapo suala la kuimarisha uhusiano na ushirikiano lilichukua nafasi kubwa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment