HISTORIA YA MARCUS AURELIUS[mfalme wa Roma]


LE0 KATIKA HISTORIA, ni blog inayokuwezesha kujua baadhi ya viongozi maarufu waliowahi kuwepo duniani ikiwa ni pamoja na kujua aina za uongozi wao na jinsi michango yao ilivyoibadili sura ya dunia na Leo katika historia tutaangalia maisha ya mfalme mashuhuri na mwanasalsafa mkubwa sana Marcus Aurelius aliyezaliwa mwaka 121 na kufa mwaka 180 Marcus Aurelius alikuwa ni mfalme wa Roma tangu mwaka 161 hadi 180 ambapo Lucius Verus alikuwa ndiye msaidizi wake mkuu na alikuwa ni miongoni mwa wafa lme shupavu watano wa mwisho kuitawala Roma ambapo alipitia vipindi vigumu sana katika utawala wake ikiwemo vita na njaa, Marcus pia alikuwa mwandishi na mwanafalsafa mkubwa sana miongoni mwa wanafalsafa waliowahi kuishi ulimwengu. Katika kipindi chake cha uongozi alipigana na falme kadhaa zikiwemo MARCOMANN, QUAD NA SARMATIANS na zote alishinda na kupelekea kutanuka na kuimarika kwa ROMA kwa kipindi hicho SANAMU YA MARCUS AURELIUS
KUZALIWA Asili ya familia ya marcus aurelius ni UCUBI mji mdogo wa kusini mwa CORDOBA huko BAETICA, familia yake ilianza kupata umaarufu mwanzon mwa karne ya kwanza baada ya yesu, Babu yake Marcus(marcus annius verus 1) alikuwa ni seneta kuanzia mwaka 73 mpaka mwaka 74 na babu yake wa pili(marcus annius verus 2) alikuwa ni mzalendo na baba yake marcus aliyeitwa Marcus annius verus alimwoa DOMITIA LUC ILLA, Verus na Lucilla walibahatika kupata watoto wawili wa kike na wa kiume ni ambao Marcus ambaye alizaliwa 26/04/121 na Annia cornificia Faustina aliyezaliwa 123 ba ada ya yesu, Inasadikika kuwa baba yao alifariki MWAKA 124 AD ambapo Marcu alikuwa na umri wa miaka 3 tu, na baada ya kifo cha baba yake Marcus alilelewa na babu yake, kupi tia babu yake, Marcus alijifunza maadili mema ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuishi vizuri na jamii iliyokuwa ikimzunguka, Katika kipindi kikubwa cha maisha yake alikuwa na mwalimu na rafiki mkubwa aliyeitwa Fronto ambaye alimfundisha elimu ya salsafa FRONTO alikuwa ni mwanasheria na kwa kipindi hicho cha mwaka 147 Roma ilikuwa chini ya utawala wa HERODE Mnamo mwaka 7, march 161 ANTONINOUS PIUS, ambaye alikuwa ni mfalme wa Roma alimkabidhi kiti cha ufalme Marcus Aurelius masaa machache kabla ya kifo chake ITAENDELEA MAISHA YA KIFALME MPAKA KIFO CHAKE



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: