Wakati msanii wa muziki wa Bongo Flava, Diamond Platnumz ameachia ngoma mbili kwa wakati moja ambazo ni Sikomi na Niache, ngoma ya kwanza imekuwa na nguvu na mapokeo makubwa kutokana na ujumbe uliomo ndani yake.
Katika ngoma hiyo ‘Sikomi’ Diamond amezungumzia maisha yake ya kimahusiano na wanawake maarufu kama Wema Sepetu, Penny na baby mama wake, Zari The Boss Lady.
Wimbo huo wenye dakika 3:58 Diamond anaeleza baada ya kupambana kwa kipindi kirefu hadi kuja kutoka kimuziki aliamini pengine maisha yake ya kimahusiano yangekuwa vizuri kitu ambacho anakiri hakijamtokea tangu pale alipokutana na mrembo kutoka Bongo Movie.
Licha ya kutomtaja mrembo huyo bila shaka anamzungumzia Wema Sepetu kwani ndiye mrembo pekee wa Bongo Movie aliyeanza kudate naye na couple yake kuwa na nguvu zaidi.
Hata hivyo katika verse ya pili ya ngoma hiyo ndipo ameweka wazi kuwa anayemzungumzia ni Wema Sepetu kwa kueleza licha ya kumpenda sana lakini bado aliusumbua moyo wake.
"Moyo aliupatia mateso siwezi kumeza siwezi tema/
Ndio maana sikushangaa ile ghafla toka CCM kwenda Chadema/"
"Moyo aliupatia mateso siwezi kumeza siwezi tema/
Ndio maana sikushangaa ile ghafla toka CCM kwenda Chadema/"
Utakumbuka February 24 mwaka huu Wema Sepetu mbele ya waandishi wa habari alitangaza kujivua uanachama kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitendo ambacho Diamond anaeleza hakushangazwa nacho.
Pia anakumbushia kitendo cha kuachana na Penny mwaka 2014 baada ya mrembo huyo kutoa mimba yake licha ya kumgharamia kila kitu hadi kumnunulia gari.
Hata hivyo anaeleza furaha yake ya kukutana na Zari hadi kupata watoto wawili lakini mwenye akajikuta akimkwaza.
Akanitunuku Zari akanizalia dume na mwali/
Nilivyo mjiga nikajitia aibu mpaka kwa vyombo vya habari/
Akanitunuku Zari akanizalia dume na mwali/
Nilivyo mjiga nikajitia aibu mpaka kwa vyombo vya habari/
Diamond kumkwaza Zari kwa kile alichoita ujinga wake ni baada ya kuzaa na Mwanamitindo, Hamisa Mobetto wakati bado ana mahusiano na Zari.
Utakumbuka baada ya uvumi kuwa mkubwa kuhusu Diamond kuzaa na Hamisa mwenye aliamua kwenda Clouds Media na kukiri kweli hilo lipo kitu ambacho anaona alijitia aibu.
Licha ya maswahibu yote aliyokumbana nayo bado hakomi katika mapenzi kama ilivyoeleza chorus ya ngoma hiyo na title yake.
Wimbo umefanyika Wasafi Records na producer aliyehusika ni Laizer ambaye amekuwa akifanya kazi nyingi za Diamond na wasanii wa label anayoimiliki, WCB.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment