CHOMBEZO: CHURA AMEMEPEVUKA ix

CHOMBEZO: CHURA AMEMEPEVUKA
NA: njenje ze ropo
WHATSAPP: 0755666796
EPSODE YA IX
Chacha ni kama hakusikia kelele zile.
"we Chacha weee!.....Chachaaaa!!" alipiga kelele J, Chacha akasimama na kuangalia upande ambao sauti imetokea.
"vipi mbona na mtoto wa watu gizani?" aliuliza J.
"mtoto anataka eti, hadi ngoma iishe ndo aongee na mimi wakati ameshanidatisha tayari" alijibu Chacha.
"nisikilize vizuri chacha, muda hauruhusu wewe kufanya hivyo sawa. unaonesha picha gani sasa kwangu?.....kwahiyo tunashindana si ndiyo?"
"hapana kaka, unajua haya mambo hayapangwi yanakuja tu yenyewe mwilini yani mtu unajikuta tu unatamani kufanya hii kitu"
"acha uboya Chacha, labda nikiwa sijakuona lakini nikikuona ujue tunazinguana kama ni mawe utanipiga mimi sawa. kwanza hivi ninavyoongea unatakiwa kumuacha huyo mtoto apotee" alikoroma J. Chacha kwa J haongei kitu, anajikuta mpole sana na hofu juu. Ikabidi amuachie yule mtoto. mtoto akasogea hadi alipo J kisha akainama ili kumuona vizuri.
"kumbe wewe ni yule kaka fundi masofa wa pale Masugulu, asante sana kaka kwa msaada wako. Halafu kumbe huyu ni mdogo wako mimi sijajua" alisema huyo mtoto lakini J hata hakuwa na muda naye, alikuwa akimsubiria tu azidi kuongea ili ampe cha kumpa lakini bahati yake akawahi kuondoka.
"Chacha eee!" aliita J hapo wakiwa mbali kidogo na ngoma hivyo sauti zilikuwa hazileti shida sana. Chacha akanyanyua shingo yake bila kuitikia akamtazama J usoni. Kinyonge sana, alikuwa amepokonywa ndege wake mkononi na kuachiwa apuruke.
"kile kitoto kidogo sana Chacha, utakuja upate kesi bure" alisema J, kauli hiyo ikapelekea Chacha kuguna.
"mh!"
"nini?" akauliza J.
"hamna kaka.....hamna......hakuna kitu!" alijibu J kwa kusuasua.
"nisikilize basi" akaendelea J.
"utanifanya nisiwe nakutuma tena kwa mademu Chacha, we unafikiri kama unaanza tabia hii itakuwaje eenh.......!!
" kaka ni leo tu haito jirudia tena na naomba unisamehe kaka" akamkatisha na kuomba radhi. J hakuwa mtu wa kukaa na mambo sana na huwa akiongea kama hivyo kaongea, harudii. Akalipotezea hilo jambo kisha akamsogeza dogo huyo kando kidogo ya barabara.
"Batuli.....nampataje Batuli Chacha, fanya mambo basi komandoo wangu kabla ngoma haijapunguza makali" alisema J. Chacha akacheka kidogo na kusema.
"we si umesema hunitumi tena sasa......!!
" kausha dogo leo ni mara ya mwisho" J akasema na kuifanya kauli ya Chacha kuishia hewani. Chacha alibaki akicheka huku akipotelea gizani, akimuahidi J kuwa muda si mrefu anakuja na windo hilo.
"weweeeeeee!, weweweeeiyaaaa!" kelele mbinja na sauti mbali mbali zilizoashiria jambo, zilimkera J lakini si kumkera kwa kumuudhi laa hasha! Kero hiyo ilikuwa kama mkereketo wa kutaka kujua nini sababu hasa ya kelele hizo. Hilo ndilo kubwa hasa lililokuwa likiupeleka moyo wake katika hali ya msukumo mkubwa wa kutaka kujua. Duara kubwa lililokuwa limetengezwa na ile tupsi ya watu mahali ngoma ilipo. Lilikuwa ni duara kubwa kweli huku taa za mfifio zikimulikiwa ndani ya duara hilo.
"kuna nini pale?" akajiuliza lakini akajikuta akigeuka mbele na nyuma kuangalia kama kuna mtu karibu. Hakukuwa na mtu. Akajishangaa ni kwanini kauliza kwa sauti kubwa na ilihali hakukuwa na mtu mwingine. Akaona hata hivyo kujiuliza huko hakutaleta suluhisho sahihi. Akajishauri aende au abaki amsubiri Chacha.
"mh!, mh!,......ngoja niende" akajishauri tena lakini cha kushangaza hakunyanyua mguu wake.
"lakini ngoja nibaki kwanza kidogo" aliposema hivyo, akajihisi hata moyo wake mwenyewe ukimcheka. Hakuwa na chaguo sahihi. Akiwa bado anasubiri hapo, mara akasikia
"Chacha bwana hebu niache nikaangalie mashindano.......sasa huku tunakwenda wapi" ilikuwa ni sauti ya mtoto wa kike ikilalamika. Ni wazi Chacha alishafanya alichotakiwa kufanya.
"kwani ukiitika wito na kukataa maneno kunaubaya?" sauti ya kiume ikamfanya J akenue kwa matumaini. Alikuwa ni Chacha.
"huyu dogo namkubali sana huwa anafanya kweli" aliwaza J.
"malizaneni mimi kazi yangu imekwisha" aliongea Chacha huku akiwa anahema lakini hakutoa nafasi ya kusikia neno la mtu yeyote yule mahali hapo, akakimbilia kule ambako duara kubwa lilikuwa limefunga. Hakuna aliyekuwa akiongea mahali hapo, kila mmoja alikuwa akimtazama mwenzake. J alikuwa haamini kama kweli mbele yake kuna mtoto mwenye sura ya urembo kama huyo. Akajikuta akifikiri mengi na kupoteza muda kwa muitwaji. Salamu pia hawakuzikumbuka kama zinathamani kwao.
"sema basi mi nataka kuwahi kwenye mashindano ya kunengua" aliongea kwa sauti ya juu kidogo huyo dada, sauti ambayo kama siyo fundi mithili ya J, unaweza kujishangaa mwili ukitikisika kwa mtetemo mwishoe lengo pia unapoteza.
"unanikalipia kama hujawahi kuniona kwenye maisha yako yote" alirudisha mashambulizi J na kumfanya mtoto huyo ainame ili kumuona huyo mtu vizuri. Mara mkono mdomoni, kicheko cha aibu butu kikajitokeza pia hakikudumu sana, mkono uliokuwa umeziba mdogo, ukatolewa, kicheko cha sauti kikateka nafasi sambamba na maneno.
"samahani J. Fundi, sijakujua hata kidogo halafu Chacha alivyo na tabia mbaya hata hakuniambia." pamoja na hayo lakini hakumpa nafasi tena J ya kuongea. Akamuwahi kwa kumwambia kuwa wataongea vizuri kwa kina, ngoja kwanza akaangalie mashindano ya kunengua. J hakuwa na jibu zuri hata kidogo na hata kama hilo jibu lingekuwepo, unafikiri angemjibu nani na wakati huo Batuli alishaondoka na kumuacha mwenyewe akiwa haelewi mtindo ule wa ahadi ni wa mkoa gani.
"sasa nimsubiri hapa hapa au nimsubiri wapi" alijiuliza kama mjinga fulani hivi.
"ukiwa mzuri tabu sa.......aaaah warembo wakishajua wanapendwa basi matokeo yake ndiyo haya, sasa tutaongea bila kupeana mahali pa kukutania, ebo!" aliwaza J. Akajikuta hatoki hapo, aliganda kama kuna amri ya kijeshi alipewa.
"ngoja....kwani siwezi kumpatia kule kule ngomani?......kule kule na nina hakikisha namuwinda hadi nijue aliko na nikishajua basi jicho langu moja yeye na jingine kwenye hayo mashindano. Alaa!" alijiaminisha kisha akapiga hatua ndefu ndefu kulifuata duara.
Ahadi inakuaminisha kuwa ulichoahidiwa kinakwenda kutimia hata kama si kwa wakati. Ni mengi tunaahidi, tunaahidiwa lakini baadhi ya hayo tunayoahidiwa, huwa si yakutimia. Je, unaweza ukajenga chuki kwayo? Jibu ni ndiyo au hapana. Nasema kuwa jibu ni ndiyo au hapana kwa sababu moja kuu, watu tuna tofautiana sana na hizi tofauti zetu ndizo zinazoleta majibu hayo mawili. Mwingine ni mwepesi sana wa kukasirika punde tu apewapo ahadi butu. Wengine huichukulia ni sehemu ya maisha na kuijumuisha kwenye changamoto za kawaida za kimaisha. Kwa nini mwandishi nimesema haya?......unataka kujua, ungependa kujua au si muhimu sana lakini si vibaya kujua pia?
Zidi kuwa nami kwenye chombezo hili la kukata na shoka la APPLE LIMEPEVUKA.
*********%%%%%%%%%%%**********
Lilikuwa ni dari jeupe kabisa kwa rangi yake ya kupendeza ya Creem, uwa zuri la kigeni lililokuwa likining'inia ambalo lilikuwa limeibeba taa ya kupendeza iwakapo na izimapo. Taa ya kigeni kabisa, taa yenye rangi mbalimbali za kuvutia. Hakuwa akitazama kitu chochote kwenye hilo dari lakini ukimtazama, waweza kusema kuwa labda alikuwa akimsifia fundi kwa jinsi alivyozipangilia rangi kwa sifa hadi kuleta mvuto ule kumbe laa! Tabasamu likamtoka kijana huyo, hapo ndipo alipopepesa macho yake kisha kuyageuzia pembeni. Ahadi, kabisaa, ahadi ya Batuli kwake ilikuwa haijatimia. Ahadi isiyo na kichwa wala miguu, ahadi ambayo ilimfanya kuwa wa mwisho kuondoka mara baada ya ngoma kuzimwa akiamini angeweza kumuona Batuli kwa muda ule. Hadi kujikuta akilala saa tisa usiku juu ya alama.
"mh hg!.......mbruuu!" alikizuia kicheko kisimtoke J baada ya kufijiri kwa kina na kujiona mjinga sana.
"hivi kweli Batuli ameniweka mimi hadi saa tisa.....siamini, kwa nini sasa?....hapana kwani ndiyo nampenda au ni kama wengine tu ambao ninapita na kuacha. Sasa kama ninapita na kuacha kwa nini ameniweka hadi muda ule. Batuli ameniteka yule mtoto.....tatizo mtoto kaumbika sana hadi kero." aliwaza J akiwa hapo hapo kitandani mida hiyo ya saa tatu asubuhi na inavyoonekana hata muda wa kuamka hakuwa akiujua vizuri siku hiyo.
"Batuli.....Batuli wewe kama ndiyo unaingia kwenye hiki chumba na kulala juu ya hiki kitanda, utanikoma nasema, simaanishi kuwa nitakulia mizizi ya Lushoto ama Handeni walla, bali nitahakikisha unanijua vizuri mimi ni nani kwenye uwanja huu wa kitanda. Lazima uingie humu Batuli....sijui ni kwa nini natamani uingie humu. huwendaaa.......!" akaishia hapo ghafla tu bila kuendelea. Sauti ya mtoto mdogo wa kike ilikuwa ikimuita huko nje. Sauti hiyo ikamfanya kubaki kimya kwa muda ili kujua kama kweli ni yeye ndiye anayeitwa huko nje. Muitaji alidhamiria. Kweli alikuwa ni yeye ndiye anayeitwa.
"nani wewe" akauliza kwa sauti ya juu"
"ni mimi kaka samahani" muitaji akajibu kwa utiifu mkubwa lakini haukumfurahisha J, ulimkera waziwazi kabisa. Kitendo cha kutolewa mawazoni ilikuwa ni dhambi kubwa sana. Akatoka nje na kukutana na sura ya mtoto wa miaka kama siyo kumi na nne kumi na sita. Alikuwa mtoto kweli japo umbo lake lilikuwa la maji maji lakini pia, kifuani alishaanza kukusanya vidakwa vya maembe ki mtindo. J akavunga kuisubiria heshima yake maana kwa umri wa yule binti lazima neno shikamoo kaka/mjomba ama vinginevyo, lingehusika, hapo haikuwa hivyo.
"unanikumbuka?" hilo ndilo neno la kwanza aliloliongea huyo mtoto bila aibu, soni wala haya" J akataharuki huku akimkazia macho yule mtoto mdogo asijue ni nini anamuonesha hapo.
"watoto wa siku hizi bwana.....badala ya kunipa heshima yangu, eti, unanikumbuka, nimkumbuke ili iweje sasa" alizungumza J akiwa ameanza kukereka.
"kwani inamaana hujui mimi na wewe tulionana wapi?" yule binti mdogo akazidi kuongea

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: