Kocha Mkuu wa Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, sasa yupo huru kuanza kukaa katika benchi la timu hiyo kutokana na kumaliza adhabu yake ya kukosa mechi tatu za Ligi Kuu Bara.Pluijm ambaye msimu uliopita alikuwa kocha wa Yanga kabla ya kupewa cheo cha ukurugenzi wa benchi la ufundi klabuni hapo, alipewa adhabu hiyo Novemba, mwaka jana kutokana na kudaiwa kuwafanyia fujo waamuzi waliochezesha mechi ya Yanga dhidi yaRuvu Shooting.Mholanzi huyo amemaliza kifungo chake katika mchezo wa juzi ambao Singida iliifunga Stand United bao 1-0 ugenini.Mholanzi huyo baada ya kutoka kifungoni, amesema anachokifanya kwa sasa ni kuitengeneza zaidi timu yake iweze kupambana na timu nyingine kama Simba na Yanga kutokana na wachezaji wake wengi kutokuwa na uzoefu na michuano ya Ligi Kuu Bara.“Nashukuru nimemaliza adhabu yangu na nitaanza kukaa katika benchi kwenye mechi yetu dhidi ya Kagera Sugar, kwa ufupi kikosi changu hakijaanza vibaya msimu huu japo wachezaji wangu wengi si wazoefu na ligi kuu.“Kazi kubwa ambayo ninayo sasa ni kuwapa uzoefu wachezaji wangu kwaniwengi si wazoefu wa ligi hii, nimekuwa hapa kwa muda mrefu na najua ligi ni ngumu, hivyo ni lazima tupambane kwa hali yoyote ile kwenye maandalizi yetu ili kutoa ushindani wa kweli kwa wapinzani wetu,” alisema Pluijm.Katika mechi zake tatu za mwanzo, Singida imeshinda mbili na kupoteza moja.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment