JUMA KASEJA ATIMKIA KAGERA SUGER


Aliyekua kipa namba moja wa Tanzania na klabu ya Simba,Yanga na Mbeya City Juma Kaseja Juma amesajiliwa na klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera.

Akithibitisha kusajiliwa kwa kipa huyo mkongwe aliyejijengea jina kubwa katika soka la Tanzania meneja wa Kagera Sugar Mohamed Hussein amethibitisha kusajiliwa kwa Kaseja.

"Moja ya mapendekezo ya kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime ni usajili wa beki mmoja kipa na mshambuliaji na tayari tumekamilisha usajili wa Beki Mohamed Faki na leo tumekamilisha usajili wa Kipa Juma Kaseja" Alisema Mohamed Hussein.

Kagera Sugar mpaka kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara Ilikua ikishika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 24 pointi moja nyuma ya Azam wanaoshika nafasi ya 3 na usajili wa dirisha hili dogo utafungwa tarehe 15 mwezi Disemba

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: