HUYU NDIO KIPA MPYA WA SIMBA AMETUA

Katika harakati zake za kuhakikisha ubingwa wa ligi kuu msimu huu unatua Mitaa ya Msimbazi,Vinara wa ligi kuu Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba wamemleta kipa mpya.Daniel Agyei amewasili jijini Dar es Salaamleo mida ya saa 7 mchana akitokea kwao Ghana na kupokelewa na aliyekua meneja wa zamani wa Simba Abbas Ally ambaye kwasasa ni mratibu wa timu hiyo.Taarifa toka ndani ya Simba zinasema kwamba Agyei atasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba ikiwa ni pemdekezo la mwalimu wa timu hiyo Joseph Omog.Moja ya maeneo yaliyoonekana kupwaya katika kikosi cha Simba msimu huu ni pamoja na nafasi ya kipa ambapo kipa namba moja Vicent Angban alikua hana mpinzani baada ya kudaka mechi zote huku akifungwa mabao ambayo baadhi ya wanasimba walihoji uwezo wake.DANIEL AGYEI NI NANI?Anaitwa Daniel Nana Agyei, Amezaliwa miaka 27 iliyopita katika kitongoji cha  Dansoma jijini Accra nchini Ghana.Ni mmoja kati ya makipa wa timu ya taifa ya Ghana akiichezea mara 5 na anajiunga na Simba akitokea Medeama ya Ghana ambao walimsajili kutoka Liberty Proffesionals ya huko huko Ghana.Ni kati ya wachezaji walioshinda ubingwa wa dunia kwa vijana chini ya miaka 20 mwaka 2009.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: