WAZEE LUDEWA WAMTEMBELEA MKUU WAO WA WILAYA

. WAPENDEZWA NA KAZI YA UTENDAJI KAZI WAKE NA KUMKARIBISHA RASMI LUDEWA.                              NAYE ATAJA MAFANIKIO NA MACHANGAMOTO ZINAZOIKABILI LUDEWA NA NAMNA ANAVYOZISHUGHULIKIA. Wamemwahidi kumpa ushirikiano lakini      wakamtaka Kuwa mwangalifu na watu kwa makundi yao wakiwepo watumishi wasioitakia mema Ludewa ,     Naye    Akitoa taarifa Kwa wazee hao Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere amesema katika kipindi cha miezi sita tu tangu afike Ludewa amekutana na changamoto nyingi na kuzishughulikia kwa kuchukua hatua ikiwemo kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri, Kuhakikisha na Wajawazito wanajifungulia katika sehemu safi na salama na kukoma kulala chini kutokana na uchakavu wa wodi yao, Kukomesha tabia ya baadhi ya watendaji wa vijiji na Kata kujifanya miungu watu kwa kuwanyanyasa Wananchi na kushindwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa wakati, kufuatilia ubadhirifu wa Tsh m. 300 kati ya sh m. 400 zilizotolewa na serikali kujenga ofisi za Halmashauri, Kubaini Ubadhirifu wa sh m. 450 za mradi wa umwagiliaji Lifua ambapo sasa waliohusika wameanza kuchukuliwa hatua, Kuhakikisha wazee wanapata haki stahiki ya matibabu bure, Halmashauri kutumia vibaya pesa kwa ajili ya mikopo kwa vijana na akina mama, Kuwaandaa Wananchi juu fursa zitakazotokana na uwekezaji katika migodi ya Liganga na Mchuchuma,Kuchukua hatua juu ya Kuporomoka kwa taaluma ya elimu ya msingi na Sekondari, Kupunguza kasi ya Maambukizi ya VVU,  Ujenzi wa viwanda vya kusaga unga, Kuleta mbegu za korosho, na kuongeza kuwa Mambo mengi aliyoyataja yapo katika hatua nzuri ya utekelezaji  na kwamba atahakikisha Ludewa mpya inapatikana kwa kushirikiana na wadau mbalilimbali wa maendeleo na kwa kila mwana Ludewa kuchapa kazi na kuacha kulalamika, ameomba pia ushirikiano kwa kila mwana Ludewa,

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: