Utafiti uliofanyika na kutolewa miezi kadhaa iliyopita na Vyuo Vikuu Vya Rice na North Texas, umegundua mambo kadhaa muhimu linapokuja suala la wanawake kupendelea zaidi kutoka na wanaume warefu. Watafiti hao walifanya utafiti katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza, waliangalia vipaumbele vya wanawake na wanaume katika suala zima la kudeti (Dating Prefences) kwa kutumia matanganzo ya mapenzi 925 (personal dating ads) yaliyowekwa Yahoo!.
Sehemu ya pili ya utafiti ilihusisha wanaume 54 na wanawake 131 kutoka chuo fulani Marekani, ambapo majibu yao kwa maswali waliyoulizwa yalidhibitisha tafiti zilizowahi kufanyika siku za nyuma. Katika majibu yao, zaidi ya nusu ya wanawake (asilimia 55 ya wanawake) walisema wanapendelea zaidi kudeti wanaume warefu, wakati asilimia 37 ya wanaume walisema wanapendelea kudeti wanawake wafupi.
Embu tuchambue kidogo…hii ina maana gani? Ina maana kwamba mambo hayapo sawia hapa (no balance), kwani wakati asilimia 55 ya wanawake wanataka wanaume warefu, ni asilimia 37 tu ya wanaume wanaotaka wanawake wafupi, angalau kwa mujibu wa utafiti huu. Kwa maana hiyo basi wanaume pia wanapendelea wanawake warefu? Tukumbuke pia idadi ya wanaume (55) waliolizwa ilikuwa ni ndogo ukilinganisha na wanawake walioulizwa (131). Poa tuendelee basi, ili tuone utafiti huu ulibaini lipi la ziada…
Kati ya wale watu 925 waliolizwa, 455 walikuwa ni wanaume wenye wastani wa umri wa miaka 36 na urefu wa futi 5 na inchi 8 (177 cm) na wanawake walikuwa 470 wenye wastani wa umri wa miaka 35 na urefu wa futi 5 na inchi 4 (165 cm). Matokeo ni kwamba, wanaume asilimia 14 tu ndio walisema wanapendelea kudeti wanawake wafupi. Hapa pia wanaume wachache sana wameonyesha kupendelea wanawake wafupi, na tukumbuke kwamba katika kundi hili idadi ya waliolizwa ilikuwa inakaribiana sana, yaani wanaume 455 na wanawake 470.
Ilipokuja kwa wanawake wale 470 walioulizwa, karibia nusu au asilimia 49 walisema kwamba wanataka kudeti wanaume warefu kuliko wao tu! Na baadhi yao walinukuliwa wakisema yafuatayo:
“Kama mwanamke, najisikia na amani zaidi (secure) [anapokuwa na mwanaume mrefu]. Nahisi kama kuna kitu akipo sawa nikifikiria kumuangalia mwanaume wangu kwa chini!” alisema mmoja wa washiriki hao. Na mwingine nae akasema..
“Kuna pia suala zima la kuvaa viatu vya mchuchumio (high heels) na wakati huohuo bado kuendelea kuwa mfupi mbele ya mwanaume wako. Na pia nataka kumkumbatia huku mikono yangu ikimzunguka shingoni”. Nafikri unapata picha jinsi jamaa alivyo mrefu kwake au sio?
Hayo ni baadhi tu ya maoni ya wale walioulizwa kwanini wanapendelea wanaume warefu, bila shaka unaweza ukafanya utafiti wako mwenyewe kwa kuuliza wanawake wachache unaowafahamu kwanini wanapendelea wanaume warefu. Sababu nyingi huwa zinajirudia (kama hii sababu ya kujihisi na amani a.k.a “secure”), lakini si ajabu unaweza ukajikuta unaibua sababu nyingine mpya lukuki!
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment