Siku moja baada ya klabu ya Simba kutangaza mkutano mkuu wa dharura kwa ajili ya kufanya mabadiko ya katiba yao, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja amesema, kama Simba imefuata taratibu na katiba yao katika kuitisha mkutano huo, BMT kwa niaba ya serikali haina tatizo na mkutano huo.
Kiganja amesema, kinachotakiwa ni taratibu kufuatwa, baada ya hapo Simba watawasilisha kwa BMT kile walichojadili kwenye mkutano wao.
“Sisi hatuwezi kuwazuia wao kukutana kama wameamua kukutana na kama ni mkutanano wa amani acha wakutane kwa amani yao wakajadili watatuletea watakayojadili. Watu wanataka kwenda kwenye mkutano hatuwezi kuwazuia kwenda kwenye mikutano yao,” amesema Kiganja wakati akijibu moja ya swali kutoka kwa waandishi wa habari.
“Sisi kama serikali tunaendelea kusema kwamba, mikutano wala siyo shida kwetu, lakini shida ni maamuzi ambayo yanaweza kuigawa klabu yao au kuwagawa wananchi, hapo ndipo hatutaki.”
“Kama taratibu zao zote zimekamilika inamaana mkutano unakwenda kwa taratibu na kama hakuna watu wanaokuja kwetu kutuambia ‘hakipo hiki hakipo kile’, sisi hatuna tatizo. Sisi tunachotaka ni kufuatwa kwa taratibu.”
Jana Jumatatu Novemba 21, kitengo cha habari na mawasiliano cha Simba SC kilitoa taarifa ya kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa klabu hiyo wenye lengo la kufanyia mabadiliko ya katiba unaotarajiwa kufanyika Desemba 11 mwaka huu kwenye bwalo la maofisa wa polisi Oysterbay, jini Dar es Salaam.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment