Mzee Ibrahim Akilimali amejitangaza mshindi wa mchakato wa mabadiliko ya kuikodisha klabu ya Yanga kutoka kwenye uendeshaji wa sasa (wanachama) kwenda kwa kampuni ya Yanga Yetu Limited ambao baadaye ulisitishwa na serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT).
Akizungumza na kituo cha rado E FM cha jijini Dar es Salaam, Mzee Akilimali amesema yeye ni mshindi wa jaribio lililotaka kufanywa la kuikodisha timu Yanga kwa kampuni ya Yanga Yetu Limited kwasababu mwisho wa siku jaribio hilo lilikwama baada ya serikali kutoa muongozo juu ya mabadilko yanayotaka kufanywa na vilabu vya Yanga na Simba kutoka mfumo wa wanachama kwenda mfumo wa kisasa wa uendeshaji.
“Kwani unasikia tena mambo ya Yanga Yetu? Mimi nilishinda kwasababu serikali ilishazuia kilichotaka kufanywa, kuikodisha timu bila kufata taratibu sahihi,” amesema Mzee akilimali ambaye alipinga kwa nguvu zote kukodishwa kwa klabu ya Yanga kutoka kwa wanachama kwenda kwa kampuni ya Yanga Yetu kwa muda wa miaka 10 akidai taratibu hazikufuatwa.
Hata hivyo katibu huyo wa baraza la wazee wa Yanga amesema, yeye hapingi mabadilko ya uendeshaji yanayotaka kufanywa ndani ya Yanga badala yake anataka taratibu za kisheria zifuatwe ili kupata mfumo utakaoipa Yanga maendeleo.
“Mimi napenda maendeleo lakini nataka taratibu zifuatwe ili mabadiliko hayo yawe na faida kwa pande zote, mwanzo nilikuwa napinga aina ya mabadiliko kutokana na kutofuatwa kwa taratibu kwasababu timu ilitaka kukodishwa kama vile mtu anakodi masufuria ya shughulini
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment