WAZIRI JAFFO ATEMBELEA NA KUNENA MAZITO HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE


IMG_2510Naibu Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jaffo akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.IMG_2580Naibu Waziri akiwa amepanga foleni katika dirisha la malipo alipokuwa kwenye ziara Hospitali ya Wilaya ya Rungwe MakandanaIMG_2587Naibu Waziri akilipia huduma dirishani katika Hospitali ya Makandana Wilaya ya RungweIMG_2607Naibu Waziri akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupewa risiti ya kawaida na sio ya kielektronikiIMG_2605Naibu Waziri akionesha risiti aliyopewa dirishani baada ya kulipia huduma na kushangazwa kuona Hospitali hiyo bado inatumia mfumo wa zamani ukusanyaji wa mapato

Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amegeuka na kuwa mbogo kwa uongozi wa Hospitali ya Makandana ya Willaya ya Rungwe, Mbeya baada ya kunusa harufu ya  ufisadi  baada ya kujionea mwenyewe uongozi wa hospitali hiyo unaendelea kutoa risiti za mkono badala ya kutumia mfumo wa kieletroniki kwenye malipo ya wagonjwa.
Jafo alifika hospitalini hapo juzi na kwenda moja kwa moja kwenye dirisha la malipo kisha akaomba kuandikishwa na kuomba risiti na muuguzi aliyekuwa akipokea malipo hayo akamuandikia na kumpatia risiti ya kuandikwa kwa mkono.
Baada ya kupokea risiti hizo akaanza ndipo alianza kuwaweka kitomotoi Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Marco Mbata na mweka hazi  wa halmashauri hiyo sababu za kutumia mfumo ambao ulishapigwa marufuku  na kuagizwa kufunga mfumo wa kieletroniki ili kudhibiti mapato.
Jafo alimuuliza mganga mkuu, Mbata  kwa mwezi wanakusanya kiasi gani, ambapo Mbata alisema wanakusanya Sh3 milioni, jambo lililonekana kuibua hasira kwa Naibu Waziri huyo akisema huo ni mpango wa kuendelea kuiba mapato kwa kuendelea risiti za mkono na kutishia kuwatimua kazi Mbata na mweka hazina wa halmashauri.
“Kwanza hii risiti yenyewe ni feki….. nilishaagiza ifikapo Julai 30 mwaka huu kila hospitali iwe imefunga mfumo wa kieletroniki, na hospitali zote zilizofunga zimeongeza mara dufu mapato yake  lakini nyinyi bado mnaendelea na mfumo huu ambao mnatumia kuiba fedha. Hapa mnakuwa kuwa na vitabu vya   risiti vyenu ambavyo mnakwepesha mapato kwa kujiingizia kwenye mifuko yenu,” alisema Jafo.
Akitoa utetezi wake,  Katibu wa Hospitali hiyo Leonard Lwesya alisema sababu ya kuendelea ni mfumo huo ni kutokana na mfadhili aliyeingiza mkataba na Wiraza ya Afya kufunga mfumo huo bado hajakamilisha japo yupo hatua za mwisho.
Naibu Waziri, Jafo hakuweza kukubaliana na utetezi huo huku akitoa siku 25 kuanzia jana wawe wamefunga na kuanza kutumia mashine za kieletroniki na  endapo itafika  Septemba 30 mwaka huu hawajafunga mfumo huo basi Mganga Mkuu na Mweka hazina wa halmashauri hiyo watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Hata alipoingia wodini kuzungumza na wagonjwa, Naibu Waziri Jafo alielezwa kwamba huduma zinazotolewa hapo hususani nyakati za usiku ni duni.
Mgonjwa aliyezungumza na Naibu Waziri Jafo, Julias Songella alisema wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo wanalazimika kila mmoja kwenda na mablanketi yake, lakini pia usiku hawapatiwi huduma nzuri kwani hata mabomba ya sindano yanakosekana.
Baada ya kusikiliza kero hizo, Naibu Waziri, Jafo alipowabana wauguzi  waliokutwa wodini hapo kwanini mabomba ya sindano yanakosana hawakuwa na majibu licha ya kukiri mbele ya Mganga Mkuu, Mbata kwamba hakuna.
“Hii yote hii inatokana na ubadhirifu wa mapato hadi mnashindwa kununua mabomba ya sindano na groves, kwa sababu fedha zinaishia mikononi mwa watu wachache. Haingii akilini kabisa eti unaniambia kwa mwezi unakusanya Sh3 milioni hospitali kubwa kama hii?…. haiwezekani hapa kuna kitu ndio maana hamtaki kufunga mashine za kieletroniki,” alisema Jafo.


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: